Akiondoa Wazee Baraza la Mawaziri ametatua tatizo?

Akiondoa Wazee Baraza la Mawaziri ametatua tatizo?

Inafaa akae chini tena atafute chanzo cha mtatizo yanaoikabili serikali yake na chama chake kwa sababu matatizo hayo hayapo katika umri wa mtu yeyote


Jamani na sisi hapa tumezidi kila siku tunalalamika kuhusu kina Kingunge & CO kuhusu umri wao, sasa leo JK anaahidi kuwatosa bado tunalamimika. Kwa hiyo tulitaka aseme mwakani kama nitashinda nitawaacha wazee wote kwenye cabinet maana uzee sio tatizo?

Mimi nadhani tunatakiwa kumsihi atekeleze jambo hilo aliloahidi maana hatuwezi kumlazimisha uteuzi uko mikononi mwake.

Bravo JK............. usinishau niko tayari kutumikia nchi yangu naahidi sitawaangusha watz
 
Hivi nahodha kama hajui anakokwenda si atafika bandari yeyote tu au ataishia kugonga mwamba, kusema atabadili mabaharia na kuweka vijana si bado kama hana anakokwenda si ataishia popote labda watamsaidia kufika huko popote haraka.

Nimependa hili
Tatizo letu sio uzee tatizo letu unataka kutupeleka wapi mpaka sasa hujui tunakotaka tuende na hivi juzi juzi ulikiri ilani za ccm ukushirikishwa kuziandaa kwa hiyo hazitekeleziki (haya yalisemwa na mwenyekiti wa chama).

Labda hiyo Ilani iliandaliwa na "wazee"; hiyo ya mwakani itaandaliwa na vijana.

Na kama ilani ya ccm sio yako na wewe ya kwako ujaweka wazi basi hapa tulipo hatukufika kwa bahati mbaya maana kuaamua au kutokuamua yote ni maamuzi hata kama hukuwa timamu katika hayo yote mawili ya kuamua au kutokuamua.

well said.

Hatuwezi kuendelea kwa kubahatisha tu. Maendeleo ya kweli upangwa na kazi kufanyika kuyafuata maendeleo hayo uliyo yapanga, unapoyalenga unaendelea kuyafuatilia mpaka uyapate.

wenzio wanaoombea maendeleo yatokee kama uyoga nyikani.


Mpaka sasa hatujui msimamo wako zaidi ya kukaaa kimya kila wakati watu wanapoitaji muongozo wako.

Hataki kulaumiwa; na wakati mwingine akizungumza ndiyo haya yanatokea!

Walau tungejua kuwa baba analia njaa na uwezo wa kutafuta chakula hana, ndio by natural law mtu mwingine angechukua madaraka yako kufanya hilo usiloliweza. Ukikaa kimya tunafikiri unatunga sheria kumbe ???????

Kikwete hana mtazamo wa namna hiyo; Nchi inapokabiliwa na njaa yeye anafikiria wawekezaji wataweza vipi kutusaidia!


Tumekuwa watu wa kulalamika tu siku zote hizi ulizoingia madarakani, wananchi wanalalamika, rais analalamika, ccm wanalamika, wapinzani wanalalamika.

Na watoto walio tumboni nao wataanza kulalamika pale Hospitali ya Temeke!

Viongozi wako wapi? Kama wote tumebaki kwenye cycle ya malalamiko. Tatizo letu kubwa hapa tanzania ni viongozi wafuasi wapo kibao wanasubiri viongozi ambao hawapo.

Nilisema huko nyuma kuwa "wameshinda kuongoza sasa wanafuata"!

Mbaya zaidi watu wote wenye mapenzi mema mmepotea hampo mmetuachia hawa watuongoze makaburini.

Watu wenye mapenzi mema ni maadui wao; ukijitokeza kutoa mwanga watakupigia kelele "anajifanya anajua sana huyu!"... Mimi naamini huko mbeleni tutangeneza uwanja wa kuwatwangia risasi kama enzi za utawala wa Rumi na wale simba kwenye coleseum!

Wale waliokuwa wanachagua viongozi wenye busara zao wako wapi? Haingii akilini kuwa na mawaziri ambao unapaswa kumfundisha kwanza aishi vipi kama mke au mume, halafu ukamwambia aende vipi kama waziri? Jama huo muda wa mafunzo hayo yote tunao?

Mwenzio alianza na semina ya Ngurdoto! Ilikuwa kama jando lililotumia wembe butu!
 
Huyu mheshimiwa inabidi aambiwe wazi kuwa tatizo la serikali yake ni yeye mwenyewe. Kama anafikiri tatizo la serikali yake ni wazee wenzake, basi na yeye aachie ngazi kwa sababu hizo hizo za uzee.

Wakuu sijui kama ni hisia zangu tu. Bali nachokiona hapa ni kampeni ambazo mkuu anaanza kuzifanya kwa kuwapumbaza vijana.
Nina wasiwasi kama ana ushahidi wowote wakuthibitisha matamshi yake
kwani katika ahadi zote alizotoa hajawahi kutimiza lolote.
Pili kuhusu la wazee nafikiri usemi huu unatokana na wasiwasi kuhusu hoja kadha ambazo wazee k.m Warioba kina Salim wamekuwa wakimwelekezea
hasa kuhusu vacuum ya uongozi wake.
 
Back
Top Bottom