Akivunja vyombo dada huwa si muangalifu lakini akivunja mother house ni bahati mbaya?

Akivunja vyombo dada huwa si muangalifu lakini akivunja mother house ni bahati mbaya?

Yani kama ikiwezekana kabisa usiwe na House Girl.. Ikishindikana kabisa kwamba lazima awepo basi awe wakuja asubuhi na kuondoka jioni asiwe wa boarding [emoji23]
Inategemea kama una watoto wadogo mmh unahitaji kuondoka asubuhi dada anakwambia ameibiwa nauli ya daladala pichu itakubana
 
Hahahaaa. Lol.

Mie naona suluhu ni kusisitiza umakini tu kwa hao wasaidizi hasa kwenye matumizi ya vyombo sababu kikawaida maisha tuliyoishi nyuma mara nyingi hatupendi yaendelee mpaka kwenye vizazi vyetu, hivyo kama ni mdada anapovunja vyombo ikiwa ni kwa bahati mbaya hapaswi kukaripiwa zaidi ya kuelimishwa kwamba mazowea siku zote hugeuka na kuwa tabia.

Hivyo akizowea kuvunja kuanzia chini basi iko siku atakuwa na kwake na ndio itakuwa tabia yake hivyo kuvunja vyombo hovyo hovyo. Na kwa waelewa huwa wanaelewa kabisa.
Kuna zile sanahani za kwa machinga zile, ninaongeza kila baada ya miezi sita. Hata wakivunja ninaangalia tu. lakini zile special wageni wakiondoka ninaosha mwenyewe
 
Kabisa. Hawa watu hata tukiwatetea aje wanamakusudi sana. Umlipe mshahara mkubwa,mtendee wema bado hawajirekebishi. Wachache sana wanaojielewa

Umeonaeee. Walio wengi huwa wananongwa.
 
ivi ni lazima kuishi na housegirl????
Majukumu na ulezi wa watoto, pia kuna wengine ndugu zake wamekukabidhi ili umuendeleze na wao pia uwakumbuke kidogo hali ni ngumu. Wengine tunawachukua ili kusaidiana
 
Kuna baadhi ya nyumba wanawatreat HGs kama lowest class citizens. Yaani hata vitoto chini ya miaka minne vinajua kabisa hawa sio level zetu kwa jinsi wanavyokuwa treated. Ndio maana wakati mwingine hawa HGs hufanya matukio ya kutisha na kusepa zao

Ukienda nao sawa wanakupanda kichwani...mtunze utakavo mtunza lakini ukiingia kwenye 18 zake lazma akupige..
 
Kuna mama mmoja alikua haruhusu hausgal anywe chai kwa kitafunio hasa wali ataacha kauchora alama zake ,watoto wakirud wanazikuta wanaula,jion mama mtu anawauliza kama walizikuta alama wakijibu ndio basi pona ya hausgel,wakijibu hapana,bidada atakula kipigo kikubwa hadi huruma
Duuh! Ila wamama wa hivyo nao.

Na hapo ukute huyo mama anaondoka asubuhi kurudi usiku, huyo huyo anayemfanyia hivyo anamwacha na watoto na saa nyingine hata chakula cha watoto na cha jioni ndio mpikaji sasa akiamua kufanya ubaya si anaufanya bila wasiwasi.
 
Kuna zile sanahani za kwa machinga zile, ninaongeza kila baada ya miezi sita. Hata wakivunja ninaangalia tu. lakini zile special wageni wakiondoka ninaosha mwenyewe
Hapo kwa ufanyalo ni sawa kabisa Dada.
 
Inategemea kama una watoto wadogo mmh unahitaji kuindoka asubuhi dada anakwambia ameibiwa nauli ya daladala pichu itakubana
Anyways mimi najua HGs wengi wanaokuwa na vituko ni kutokana na the way unavyoishi nae. Sisi kwetu tokea tukiwa makidi wadogo tulikua na HG huyo katulea mpaka tumekuwa madingi tunaishi fresh sana mpaka amekuja kuondoka tukiwa secondary lakini ni kama member wa family hakujawahi kuwa na quarrel yoyote miaka karibia 20..

Mkiwa mnaishi na HG vizuri wala hakutakuwa na shida. Unaweza kumwachia watoto hata mwezi ukasafiri ukarudi ukakuta kila kitu kipo yechu.

Tatizo wamama wengi wa siku hizi midomo mirefu kama kunguru. Mtu akikosea kidogo wanasahau kuwa ni binadamu kama wao. Atasemwa, atasutwa, atapigwa, atatukanwa. Unategema huyo mtu ataishi vizuri na wewe kwa manyanyaso hayo? Never.

Kuweni na ubinadamu mchukulie yule HG kama mwanao. Akikosea mwelekeze na sio umpige au kumtukana. Jenga uaminifu na upendo kwake. Ukijidai kumtesa na manyanyaso hakawii kumng'oa mwanao kucha bila ganzi
 
Ukienda nao sawa wanakupanda kichwani...mtunze utakavo mtunza lakini ukiingia kwenye 18 zake lazma akupige..
Kweli kabisa Mkuu. Wadada kuweza kuishi nao hawapaswi kujua mwenye nyumba ana rangi gani yaani penye kubadilika unambadilikia na pia hawapaswi kuaminika kwa 100% hata siku moja.

Sababu waeza kuta unaishi naye kama ndugu ila yeye kwenye ule undugu amejitoa kabisa.
 
Kweli kabisa Mkuu. Wadada kuweza kuishi nao hawapaswi kujua mwenye nyumba ana rangi gani yaani penye kubadilika unambadilikia na pia hawapaswi kuaminika kwa 100% hata siku moja.

Sababu waeza kuta unaishi naye kama ndugu ila yeye kwenye ule undugu amejitoa kabisa.
Ila cha moto wanakiona wale wanaofanya kazi kwenye nyumba za wahindi...No chai 😀😀
 
wengine wanalawama akivunja mtu analaumu akivunja yeye anamlaumu aliyeweka pale kile chombo

utasikia nani kaweka glasi juu ya meza umeona umesababisha imevunjika
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Mbaazi ikikosa maua....
 
Ila cha moto wanakiona wale wanaofanya kazi kwenye nyumba za wahindi...No chai 😀😀
Ila wale si nasikia hawalalagi yaani ni kama Mfanyakazi wa Ofisi nyingine, kwamba unaenda kufanya kazi tu ila kila kitu juu yako.

Ikifika mida ya kuondoka unakwenda nyumbani. Au sivyo nijuavyo Mkuu?
 
Back
Top Bottom