Akopea nyumba ya jirani Milioni 200 kwa Hati Feki. Malalamiko yalifika hadi Ikulu danadana nyingi

Akopea nyumba ya jirani Milioni 200 kwa Hati Feki. Malalamiko yalifika hadi Ikulu danadana nyingi

toriyama

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2014
Posts
1,139
Reaction score
2,223
Mtu mmoja ambaye ametajwa kwa jina la Mkwabi Nyanda akishirikiana na Mkewe wanadaiwa kugushi nyaraka za hati ya nyumba ya Jirani yao eneo la Kinondoni Jijini Dar es salaam na kutumia hati feki kukopea benki Jijini Arusha Tsh. milioni 150 mwaka 2016 na kisha milioni 200 mwaka 2017 na kupelekea benki hiyo sasa kutaka kuuza nyumba huku Familia inayomiliki nyumba hiyo ikisema haihusiki na mkopo huo wala haiutambui.

Kijana Dotto Said(19) ambaye nyumba hiyo ni ya Babu na Bibi yake amesema katika mapambano ya kuinusuru nyumba ya Familia isiuzwe amefika hadi Ikulu kupeleka barua aliyomuandikia Rais ambako aliambiwa Rais ameiona barua yake na ameagiza aiandike barua kama hiyo kwa Waziri wa Ardhi (nakala iende TAKUKURU, kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, kwa IGP na DPP) ili atatuliwe shida yake haraka kwakuwa tayari benki imewataka waondoke ili nyumba iuzwe kwakuwa Mahakama imetoa maamuzi kuwa benki iuze nyumba hiyo.

Dotto amesema “Tulishafungua kesi ya kugushi kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay (Dar es salaam), baada ya upelelezi Mtuhumiwa akabainika yupo Arusha, Polisi wakataka Tsh. milioni 1.5 kwenda kumkamata Arusha tukawapa wakaenda na gari Dogo Askari watatu wakamkamata wakati wanarudi nae kuja Dar es salaam Askari wanasema wamefika Mombo Hotelini Mtuhumiwa alikuwa ananuka wakamwambia aende chooni akajisaidie baadaye akatoroka kupitia dirishani”

“Wakarudi Arusha kumkamata Mkewe na walipofika Dar Mke akakiri kwenye mkopo benki waligushi ambapo yeye alisimama kama Zainab (Bibi yangu) na Mumewe akasimama kama Abraham (Babu yangu) lakini baadaye Mke kaachiwa, ombi langu tunaomba benki ituachie nyumba yetu, benki imtafute aliyewatapeli kwasababu yupo, tunamuomba Mh.Rais, Waziri na Watanzania wote watusaidie”

Baada ya Ayo TV kurusha habari hii kwa urefu kwenye Youtube ya MilardAyo siku chache zilizopita, leo July 01,2024, Dotto amesema wameitwa kukutana na Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa ofisini kwake na amewaahidi kuwasaidia wapate haki yao “Tunaishukuru Ayo TV, tumeonana na Waziri amesema ameiona habari Ayo TV na pia nimeambiwa Rais Dkt. Samia nae ameiona habari Ayo TV na ameagiza kwa msisitizo tusaidiwe, nitawajulisha jambo litakapofikia na kitakachojiri”


 
Hili sio Kosa la kwanza kuna mtu nae ilitokea huko kanda ya ziwa sema nae alikua yuko vizuri na eneo lake lilikua na hati original hivyo Bank wao ndio walibaki wanajiuliza walitoaje mkopo kwa Hati ya Kughushi?
 
Hili sio Kosa la kwanza kuna mtu nae ilitokea huko kanda ya ziwa sema nae alikua yuko vizuri na eneo lake lilikua na hati original hivyo Bank wao ndio walibaki wanajiuliza walitoaje mkopo kwa Hati ya Kughushi ?

Kwa zama hizi huwezi kutengeneza hati mbili kwenye kiwanja kimoja. Database inakataa kutoa hati ya pili.

Jamaa alifanya zama za zamani zamani kabla ya hati zote kuingizwa kwenye system
 
Hapa ndipo ule msemo wa mficha uchi hazai unapodhihirika kuwa kweli.
Kabisa.
Mfano, suala kama hili badala ya kuwapa polisi 1.5M, lipa vyombo vya habari wakuhoji, andika barua ya wazi kwenye gazeti. Lipa blog uchwara wale wa mitandaoni wenye followers walaani, Yaani tengeneza atention kwa wanasiasa kutaka kupata credit kupitia tatizo lako.
 
Kabisa.
Mfano, suala kama hili badala ya kuwapa polisi 1.5M, lipa vyombo vya habari wakuhoji, andika barua ya wazi. Lipa blog uchwara wale wa mitandaoni wenye followers walaani, Yaani tengeneza atention kwa wanasiasa kutaka kupata credit ya kuisaidia jamii.

Kabisa. Ukute hao polisi wamekula 15 ya wahanga na kwa mtuhumiwa wakajichukulia chao vile vile.
 
kabisa. Ukute hao polisi wamekula 15 ya wahanga na kwa mtuhumiwa wakajichukulia chao vile vile.
Unapoteza pesa na husaidiki. Kama unajua suala lako halina utata ni kweli unatapeliwa itafute huruma ya jamii ila kama kuna utata ila unatapeliwa hapo tumia hizo mbinu za kimtaa ukijumuisha polisi na wahuni ila usichukue roho ya mtu au kisicho chako, chukua haki yako tu, maana kuna watu wanakutapeli nyaraka kwanza halafu ndo unatapeliwa mali yako. Sasa hawa ukitumia njia za kawaida hufanikiwi.
 
1.Polisi wakataka Tsh. milioni 1.5 kwenda kumkamata Arusha

2.“Wakarudi Arusha kumkamata Mkewe na walipofika Dar Mke akakiri kwenye mkopo benki waligushi ambapo yeye alisimama kama Zainab (Bibi yangu) na Mumewe akasimama kama Abraham (Babu yangu) lakini baadaye Mke kaachiwa,

POLISI NA BANK HUSIKA KUNA ULAZIMA WA KUTOA MAELEZO YENU NA NINYI
 
Back
Top Bottom