Akopea nyumba ya jirani Milioni 200 kwa Hati Feki. Malalamiko yalifika hadi Ikulu danadana nyingi

Akopea nyumba ya jirani Milioni 200 kwa Hati Feki. Malalamiko yalifika hadi Ikulu danadana nyingi

Kwa zama hizi huwezi kutengeneza hati mbili kwenye kiwanja kimoja. Database inakataa kutoa hati ya pili.

Jamaa alifanya zama za zamani zamani kabla ya hati zote kuingizwa kwenye system
Pamoja na hayo. Kuna vitu vinazidisha maswali. Kama hao mume na mke waligushi hiyo hati, kwa nini mahakama iamuru nyumba iuzwe wakati mwenye nyumba hahusiki kabisa? Yaani watu wagushi hati ya nyumba yangu, wakopee fedha, halafu mahakama ione waliogushi ndiyo wenye haki?
 
1.Polisi wakataka Tsh. milioni 1.5 kwenda kumkamata Arusha

2.“Wakarudi Arusha kumkamata Mkewe na walipofika Dar Mke akakiri kwenye mkopo benki waligushi ambapo yeye alisimama kama Zainab (Bibi yangu) na Mumewe akasimama kama Abraham (Babu yangu) lakini baadaye Mke kaachiwa,

POLISI NA BANK HUSIKA KUNA ULAZIMA WA KUTOA MAELEZO YENU NA NINYI
Kabisa. Hivi kazi ya kukamata mtu aliyegushi hati ya nyumba yangu ni ya mimi mwenye nyumba? Yaani tapeli yuko mtaani, agushi hati ya nyumba yangu bila mimi kujua, akopee fedha, halafu mimi ambaye sijui chochote ndiyo niwajibike! Kosa ni la benki kutokuwa makini kuhakikisha mwenye nyumba ni nani na hati kama ni ya kweli.
 
Polisi wahuni sana.wanakula pesa ya Nini Sasa.Benki nao ni vilaza kwelikweli.wanashindwa Nini kutambua kuwa hii ni hati original ?
Hapa kuna kitu kinafichwa. Hakuna namna mwenye nyumba anahusika mpaka apewe kazi ya kukamata matapeli.
 
wanarudi nae kuja Dar es salaam Askari wanasema wamefika Mombo Hotelini Mtuhumiwa alikuwa ananuka wakamwambia aende chooni akajisaidie baadaye akatoroka kupitia dirishani”
Polisi wana mambo ya hovyo sana
 
Mtu mmoja ambaye ametajwa kwa jina la Mkwabi Nyanda akishirikiana na Mkewe wanadaiwa kugushi nyaraka za hati ya nyumba ya Jirani yao eneo la Kinondoni Jijini Dar es salaam na kutumia hati feki kukopea benki Jijini Arusha Tsh. milioni 150 mwaka 2016 na kisha milioni 200 mwaka 2017 na kupelekea benki hiyo sasa kutaka kuuza nyumba huku Familia inayomiliki nyumba hiyo ikisema haihusiki na mkopo huo wala haiutambui.

Kijana Dotto Said(19) ambaye nyumba hiyo ni ya Babu na Bibi yake amesema katika mapambano ya kuinusuru nyumba ya Familia isiuzwe amefika hadi Ikulu kupeleka barua aliyomuandikia Rais ambako aliambiwa Rais ameiona barua yake na ameagiza aiandike barua kama hiyo kwa Waziri wa Ardhi (nakala iende TAKUKURU, kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, kwa IGP na DPP) ili atatuliwe shida yake haraka kwakuwa tayari benki imewataka waondoke ili nyumba iuzwe kwakuwa Mahakama imetoa maamuzi kuwa benki iuze nyumba hiyo.

Dotto amesema “Tulishafungua kesi ya kugushi kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay (Dar es salaam), baada ya upelelezi Mtuhumiwa akabainika yupo Arusha, Polisi wakataka Tsh. milioni 1.5 kwenda kumkamata Arusha tukawapa wakaenda na gari Dogo Askari watatu wakamkamata wakati wanarudi nae kuja Dar es salaam Askari wanasema wamefika Mombo Hotelini Mtuhumiwa alikuwa ananuka wakamwambia aende chooni akajisaidie baadaye akatoroka kupitia dirishani”

“Wakarudi Arusha kumkamata Mkewe na walipofika Dar Mke akakiri kwenye mkopo benki waligushi ambapo yeye alisimama kama Zainab (Bibi yangu) na Mumewe akasimama kama Abraham (Babu yangu) lakini baadaye Mke kaachiwa, ombi langu tunaomba benki ituachie nyumba yetu, benki imtafute aliyewatapeli kwasababu yupo, tunamuomba Mh.Rais, Waziri na Watanzania wote watusaidie”

Baada ya Ayo TV kurusha habari hii kwa urefu kwenye Youtube ya MilardAyo siku chache zilizopita, leo July 01,2024, Dotto amesema wameitwa kukutana na Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa ofisini kwake na amewaahidi kuwasaidia wapate haki yao “Tunaishukuru Ayo TV, tumeonana na Waziri amesema ameiona habari Ayo TV na pia nimeambiwa Rais Dkt. Samia nae ameiona habari Ayo TV na ameagiza kwa msisitizo tusaidiwe, nitawajulisha jambo litakapofikia na kitakachojiri”


View attachment 3030557
Dogo ni darasa la saba D lakini anajieleza vizuri
 
Pamoja na hayo. Kuna vitu vinazidisha maswali. Kama hao mume na mke waligushi hiyo hati, kwa nini mahakama iamuru nyumba iuzwe wakati mwenye nyumba hahusiki kabisa? Yaani watu wagushi hati ya nyumba yangu, wakopee fedha, halafu mahakama ione waliogushi ndiyo wenye haki?
Mahakama haina ujuzi wa kutambua nyaraka feki

Sent from my SM-G970U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom