Al Ahly 1-0 Simba | CAFCL | Al Salam Stadium

Al Ahly 1-0 Simba | CAFCL | Al Salam Stadium

MAKULUGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Posts
7,828
Reaction score
10,527
Leo ndio leo!
Wanaume wa shoka wanakutana kutafuta Nani mbabe!
Timu zote zimeshafuzu Robo Fainali, kinachosubiriwa ni Nani ataibuka mbabe baina yao, kwa kuwa mechi ya Leo haitabadilisha msimamo wa kundi. Simba inaingia uwaanjani ikiwa na Nia moja tu, kuendelea kujijenga kuwa Timu Kubwa Afrika.
Upande wao Al Ahl wao watakuwa na kazi kudhihirisha kuwa wao hi miamba ya soka Afrika.
Tujongee karibu tuone wanume Hawa wakitoana jasho
=======

00'Mwamuzi anapuliza kipenga kuashiria mwanzo wa mchezo

9' Luis anaangushwa wakati akielekea ndani ya box la Al Ahly

11' Cloutus Chama anapiga mpira wa adhabu lakini haujazaa matunda na kusababisha Counter attack ya Mohammed Sharif ambayo nayo haijazaa goli

21' Mohammed Shariff almanusa aiandikie Al Ahly goli la kwanza lakini mpira unakwenda nje kidogo ya lango

24' Inatokea piga nikupige kwenye goli la Simba, Al Ahly wanashindwa kubadilisha ubao

27' Aishi Manula anafanya jitihada kuzuia mpira na kuzaa kona ambayo haijatoa matunda kwa Al Ahly

31' Mohammed Shariff anaipa Al Ahly bao la kuongoza baada ya mabeki wa Simba kushindwa kuondoa mpira kwenye eneo la hatari

45+2' Mapumziko

46' Kahata anaingia kuchukua nafasi ya Larry Bwalya

53' Mzamiru Yassin anaingia kuchukua nafasi ya Jonas Mkude

81' Mugalu anaingia kuchukua nafasi ya Nyoni

86' Luis anaachia mkwaju mkali na kugonga mwamba wa juu

86' El Shanawy anapewa kadi ya njano baada ya kumlalamikia mwamuzi kuchezewa ndivyi sivyo kwenye eneo lake

90+3' Mpira umekwisha, Al Ahly wanaibuka kidedea kwa kuichapa Simba goli moja kwa sifuri


======

KWENGINEKO

FT' AS Vita 3-1 Al Merrick
 
Bado dk chache nchi iingie kwenye aibu kubwa
 
Halafu inakuwaje Morison anaonekana yupo Bench wakati ana njano na alitakiwa akose match hii? Sielewi mie
 
Kaena hapo mtulie muone kati Mugalu na MK14 nani striker na nani gogo.
 
simbasctanzania-20210409-0001.jpg
 
Back
Top Bottom