Natafuta Ajira
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 9,016
- 24,650
Nimeangalia mechi zote mbili za AFL zilizowakutanisha hawa waarabu na simba. Mpira niliouona upande wa al ahly sikutegemea kabisa, kiwango chao kilikua chini ya nilivyotarajia ingawa bado nahisi uenda kuna sababu ipo nyuma ya pazia kwa wao kucheza vile. Nimeiangalia hii mechi katika pande tatu.
Kwanza, Inawezekana hawa jamaa hawatishi kama tunavyowafiria. Mpira walioucheza ni wa kawaida sana, ile sio timu inayojumuisha wachezaji walionunuliwa kwa mabilioni ya hela lakini bado akili inakataa kumbuka wale ni mabingwa wa Afrika.
Upangaji matokeo. Kama uliangalia vizuri jinsi al ahly alivyokua anacheza unaweza kuona kulikua na harufu ya upangaji matokeo. Yalishatolewa maagizo mechi iishe sare. Waarabu walikosa goli nyingi za wazi cha kushangaza wakifungwa na kuwa nyuma kwa magoli wanakua aggresive na wanachomoa fasta na kiurahisi kabisa halafu wanaupooza tena mchezo kama mwanzo.
Kucheza na saikolojia ya yanga. Al ahly ana mechi mbili za group stage dhidi ya yanga, nina wasiwasi labda aliamua kucheza vile kuwapumbaza yanga waamini watacheza na timu ya kawaida tu hii itawapunguzia yanga umakini wakati wa mechi na kufungika kirahisi. Ushauri wangu kwa yanga wasiwachukulie poa hawa waarabu uenda siku ya mechi wakakutana na al ahly nyingine yenye njaa ya ushindi tofauti na ile iliyocheza na simba.