Al ahly vs simba. Waarabu hawatishi kama tunavyowafikiria, matokeo yalipangwa au walicheza na saikolojia ya yanga?

Al ahly vs simba. Waarabu hawatishi kama tunavyowafikiria, matokeo yalipangwa au walicheza na saikolojia ya yanga?

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2020
Posts
9,016
Reaction score
24,650
Nimeangalia mechi zote mbili za AFL zilizowakutanisha hawa waarabu na simba. Mpira niliouona upande wa al ahly sikutegemea kabisa, kiwango chao kilikua chini ya nilivyotarajia ingawa bado nahisi uenda kuna sababu ipo nyuma ya pazia kwa wao kucheza vile. Nimeiangalia hii mechi katika pande tatu.

Kwanza, Inawezekana hawa jamaa hawatishi kama tunavyowafiria. Mpira walioucheza ni wa kawaida sana, ile sio timu inayojumuisha wachezaji walionunuliwa kwa mabilioni ya hela lakini bado akili inakataa kumbuka wale ni mabingwa wa Afrika.

Upangaji matokeo. Kama uliangalia vizuri jinsi al ahly alivyokua anacheza unaweza kuona kulikua na harufu ya upangaji matokeo. Yalishatolewa maagizo mechi iishe sare. Waarabu walikosa goli nyingi za wazi cha kushangaza wakifungwa na kuwa nyuma kwa magoli wanakua aggresive na wanachomoa fasta na kiurahisi kabisa halafu wanaupooza tena mchezo kama mwanzo.

Kucheza na saikolojia ya yanga. Al ahly ana mechi mbili za group stage dhidi ya yanga, nina wasiwasi labda aliamua kucheza vile kuwapumbaza yanga waamini watacheza na timu ya kawaida tu hii itawapunguzia yanga umakini wakati wa mechi na kufungika kirahisi. Ushauri wangu kwa yanga wasiwachukulie poa hawa waarabu uenda siku ya mechi wakakutana na al ahly nyingine yenye njaa ya ushindi tofauti na ile iliyocheza na simba.
 
Njaa yakufunga walikuwanayo sana tu kufunga na kurudishiwa ni uzembe wa Simba yenyewe! Huyu kocha wenu wa Simba anaruhusu sana magoli angalia hata mechi nyingi za humu ndani Simba anashinda lkn nayeye kwenye mechi nyingi anafungwa yani goli lake halitoki bila kuguswa!.

Al ahly walikuwa makini ktk mechi yao ya juzi kwani ushindi tayari ulikuwa kwao maana walikuwa wanafaida ya goli mbili za ugenini!,hivyo ushindi kwao kulihitaji sare yoyote.. Simba hakuwa nachakupoteza zaidi ya kwamba alihitajika lazima afunge hivyo al ahly angeleta uzembe wowote ule basi lingemkuta jambo!. Hata alipofungwa alitulia na kufanikisha kurudisha sare ambayo ilikuwa upande wake!.

Goli la Simba kule misri lingewatangazia ushindi Simba laiti kama wangefunga dakika za mwishoni au dakika za nyongeza,lkn kwa muda ule waliopata goli kuliwafanya al ahly apate muda wakujipanga nakufanya kitu na navyoijua Simba yasasa haina ukuta mzuri sana wakutunza goli lake!.

Hakuna kilichopangwa ila mipango mikali ilikuwa kwa Al ahly kwani alidhamiria ingempa favour kwa kupata goli lolote la ugenini na ndicho alichokifanya.

Simba goli lenu linamatobo sana nafikiri Kuna kitu chakufanya juu ya hilo.
 
Ahly ndio hiyo hiyo tu, sisi wenyewe ndio tumeshindwa kulinda goli, wakitangulia wanakuwa na mchecheto. Uto wanaweza kupata hata 4 points
 
Njaa yakufunga walikuwanayo sana tu kufunga na kurudishiwa ni uzembe wa Simba yenyewe! Huyu kocha wenu wa Simba anaruhusu sana magoli angalia hata mechi nyingi za humu ndani Simba anashinda lkn nayeye kwenye mechi nyingi anafungwa yani goli lake halitoki bila kuguswa!.

Al ahly walikuwa makini ktk mechi yao ya juzi kwani ushindi tayari ulikuwa kwao maana walikuwa wanafaida ya goli mbili za ugenini!,hivyo ushindi kwao kulihitaji sare yoyote.. Simba hakuwa nachakupoteza zaidi ya kwamba alihitajika lazima afunge hivyo al ahly angeleta uzembe wowote ule basi lingemkuta jambo!. Hata alipofungwa alitulia na kufanikisha kurudisha sare ambayo ilikuwa upande wake!.

Goli la Simba kule misri lingewatangazia ushindi Simba laiti kama wangefunga dakika za mwishoni au dakika za nyongeza,lkn kwa muda ule waliopata goli kuliwafanya al ahly apate muda wakujipanga nakufanya kitu na navyoijua Simba yasasa haina ukuta mzuri sana wakutunza goli lake!.

Hakuna kilichopangwa ila mipango mikali ilikuwa kwa Al ahly kwani alidhamiria ingempa favour kwa kupata goli lolote la ugenini na ndicho alichokifanya.

Simba goli lenu linamatobo sana nafikiri Kuna kitu chakufanya juu ya hilo.

MBONA MAMBO MENGINE HAYAHITAJI HATA SHULE.

KIPAA NO 1
AISHI MANULA.

KIPA Nambari mbili Beno kakolanya ALIONDOKA ki magumashi.

KIPA Namba Tatu Ally SALUM
Kila siku Lazima AFUNGWE.

KIPA Namba 200
AYOUB MDAKA MAPANZI.

SHIDA NI UONGOZI KULETA WACHEZAJI WABOVU,VIONGOZI NI (WEZI)
 
Huyo kipa namba mbili beno kakolanya alikuwa na ubora gani mkuu.
 
Hiyo mechi Al Ahly alitumika na makampuni ya kamari kuhadaa wacheza kamari. Timu ya Simba ina udogo gani mpaka ya kuwekea odds 20 mpaka 20+?
Mashindano makubwa kama haya tena inahusisha top 8 lakini bado timu inadogoshwa kwa kiwango kikubwa kiasi hiko haiingii akilini.
Hakuna mechi yoyote kwenye hii michuano ambayo timu imepewa hata odds 10 za kushinda lakini ni Al Ahly vs Simba imefanywa hivyo?

Kwanini accuracy ya wachezaji wa Al Ahly ilikuwa ndogo uwanjani hasa kwenye final third ya Simba? Bora hata wangekuwa wanapiga mipira kulenga golini tungesema uimara wa kipa lakini wao kule mbele kila mshambuliaji akipata nafasi anapaisha juu utafikiri wachezaji wa timu ndogo kumbe ni professional kabisa.
Hawajui kupiga penetration pass za kutengeneza magoli lakini wakifungwa tu wana react haraka na hawafanyi makosa wanarudisha tena kwa nafasi finyu wanayoipata wakati hapo kabla walikuwa wanajibutulia tu mpira juu ya lango.
 
Back
Top Bottom