Al Ahly yamtimua kocha siku moja baada ya Mamelodi kuwatibulia CAFCL

Al Ahly yamtimua kocha siku moja baada ya Mamelodi kuwatibulia CAFCL

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Klabu ya Al Ahly imemtimua kocha wake, Marcel Koller siku moja baada ya timu hiyo kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Aprili 26, 2025 uongozi wa Al Ahly umethibitisha kuwa umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Koller, ambaye aliiongoza timu hiyo kwa misimu miwili, ikiwemo kuisaidia kutwaa taji la Afrika.

"Baada ya tathmini ya kina kufuatia matokeo dhidi ya Mamelodi, bodi ya klabu imeamua kuachana rasmi na kocha Marcel Koller," imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Al Ahly iliondolewa jana Ijumaa Aprili 25, kufuatilia sare ya bao 1-1 nyumbani katika nusu fainali hiyo huku Mamelodi wakifukuzu kwa faida ya bao la ugenini baada ya mchezo wa awali Afrika Kusini kumalizika kwa suluhu.

Koller, ambaye ni raia wa Uswisi, ameondoka akiwa ameacha rekodi ya kutwaa mataji manne akiwa na Al Ahly, ikiwemo Ligi Kuu ya Misri, Kombe la Misri, Super Cup ya Afrika na Ligi ya Mabingwa 2022/23.
 
Mamelodi kipindi cha pili waliupiga sanaa, nafasi nyingi sana walitengeneza. Walitawala mpira sana ile second half.
Yaani Al Ahly yupo nyumbani anapaki bus utafikiri anaongoza goli 3 walipo ruhusu goli ndio wanaamka. Ule mpira waliocheza wakati wameruhusu goli, wangeucheza huo mchezo tokea dakika ya kwanza wangeshinda mechi.

Utofauti wa Mamelodi na Al Ahly kwenye kufanya mashambulizi ni kasi, Al Ahly wanaenda kwa kasi na kwa pasi chache wapo golini ila Mamelodi mpira wao ni pasi nyingi hivyo kwa mpira wa piga nikupige ni rahisi sana Al Ahly kufaidika na counter attack kuliko Mamelodi
 
Ahly wajinga baada ya kucheza mpira wanapak basi kwa nn usifanye makosa waxgezaji wazuri wanawaweka after kufungwa goli
 
Back
Top Bottom