Dakika 7:
Juko Marshid anamfanyia foul Islam Issa wa Al-Masry katika pembe ya kushoto ya penalt box ya lango la Simba .
Adhabu inapigwa kwenda kwa Simba na inambabatiza mtu Shagari Kapombe na kutoka nje. Kapombe shuti kali linampata kichwani yupo chini akipata huduma ya kwanza. Simba kapona Sasa ni goli kiki .
Dakika ya 11:
Mchezaji wa Al-Masry an akaendelea chini na kugaaga, Dakika zinapita na benchi la Al- Masry wakaamua kufanya mabadiliko ya mchezaji.
Dakika 13:
Aristide Bancé anachukua nafasi ya mchezajI wa Al- Masry aliyeumia, uwanja unazizima kumshangilia nyota wao raia wa Burkina Faso.
Dakika 45:
Half time mapumziko Al-Masry 0 - Simba 0. Naona wachezaji wa Simba wakikumbatiana, kupongezana na kushukuru kumaliza ngwe ya kwanza ya mechi ya leo bila kuruhusu goli. Tutarudi tena JF kuendelea kuwapatia maendeleo ya mechi hii ya kufa au kupona Al-Masry vs Simba
. Tukirudi uwanjani tutajiunga moja kwa moja na mwana-JF aliyepo uwanjani Port Said, Misri Kunguru Mjanja aendelee na matangazo mubashara.