Al Shabab wavamia mji wa Mandera Kenya

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411

Kundi la wanamgambo wa al-Shabab limevamia eneo la Omar Jillo lililoko mji wa Mandera unaopakana na Somalia usiku wa kuamkia leo.

Al-Shabab limemuua afisa huyo, Chifu ws eneo Dekow Adan na kuwateka maafisa wawili wa kitengo cha polisi wa akiba kabla ya kukimbia nchini Somalia.

Vyombo vya habari vya al-Shabab vimethibitisha uvamizi huo uliotekelezwa takriban saa nne za usiku.

Serikali ya Kenya imewatuma maafisa zaidi wa usalama hadi eneo hilo huku viongozi wa usalama wakifanya mkutano wa dharura kufuatia tukio hilo.

Mji huo wa Mandera umewekewa marufuku ya kutotoka nje baada ya saa kumi na mbili jioni kufuatia ongezeko la uvamizi kutoka kundi hilo.

Tukio hilo linajiri wiki moja tu baada ya watu wawili kuuwawa katika shambulio linalodaiwa kutekelezwa na Al shabaab.

Visa vya utovu wa usalama vimepungua eneo hilo tangu serikali ilipoweka maafisa zaidi wa uslama.

Chanzo: BBC Swahili
 
hivi hawa al shabaab huwa wanahitaji nini hasa?
as well as hayo makundi yote ya kigaidi mostly waisilamu sometimes wanauwana wao kwa wao ?
huwa wanagombea nini?
HV ughty unakitambua hicho unacho kihoji?
 
Hao wakenya ngoja waumie tu...
Wao walijipendekeza kwa kufuatana na baba wa magaidi USA.
 
hivi hawa al shabaab huwa wanahitaji nini hasa?
as well as hayo makundi yote ya kigaidi mostly waisilamu sometimes wanauwana wao kwa wao ?
huwa wanagombea nini?
Majinga tu, hayana Akili, ni kama mavichaa Fulani hivi yenyewe yanadhani yameletwa dunia yafe tu, wala sio kuishi,kuoa, kujenga, wala kujumuika na walimwengu, kiufupi ni vichaa hata haweleweki wanataka nini.
 
hivi hawa al shabaab huwa wanahitaji nini hasa?
as well as hayo makundi yote ya kigaidi mostly waisilamu sometimes wanauwana wao kwa wao ?
huwa wanagombea nini?
Vry simpl3 all they need ni kenya kuondoa majeshi yao somalia thats it.....alshabaab always fights with people who interfere with their affairs period .......
 
Hii ni hatari sana. Inabidi EAC na wengine tuangalie jinsi ya kusaidia jinsi ya kuleta amani kwenye eneo letu.
Inasikitisha kuona ka kikundi ka watu wanatishia maisha yetu sote.
 
hivi hawa al shabaab huwa wanahitaji nini hasa?
as well as hayo makundi yote ya kigaidi mostly waisilamu sometimes wanauwana wao kwa wao ?
huwa wanagombea nini?
Wanataka dunia itawaliwe na SHARIA LAWS. Hususani wenye itikadi Kali.
 
Al-Shabab, Al-Qaida, Boko haram, na magaidi wengine wanataka kuitawala dunia, yaani waunde Serikali ya dunia isiyochaguliwa kwa hiari na wananchi.
Ni kama waasi wanaotaka kuipindua serikari ya nchi ili wawe watawala.
Wakisha chukua utawala wa dunia wanataka wawasilimishe watu wote wawe Waislamu. Baada ya hapo wanataka watu waishi kwa kufuata maagizo ya dini ya Kiislamu yaliyoandikwa kwenye Quran na hadithi za mtume Mohammad.
Ni wapigania dini.
Wazo lao sio la Waislamu wote.
Na huwa wanawaua Waislamu ambao wanadhani hawafuati maagizo ya mtume Muhammadi, wenyewe wanawaita wasaliti wa
dini.
Hao ni magaidi na hawana mahusiano yoyote na Waislamu waliostaarabika.
Wanatumia mgongo wa dini kufanya maovu yao.
 
hivi hawa al shabaab huwa wanahitaji nini hasa?
as well as hayo makundi yote ya kigaidi mostly waisilamu sometimes wanauwana wao kwa wao ?
huwa wanagombea nini?
Sunni wanawaona waislam wengine kuwa ni makafir na kikwazo kwa kuenea uislam! Magaidi wanaopigania dola ya kiislam kila mahali ni sunni! Hawa jamaa ni hatari sana. Kibaha maili moja wana msikiti wao unaojulikana kama al-kaida na ni chuo pia cha kuwafundisha vijana wadogo imani hiyo! Ndio maana wahanga wakubwa wa ugaidi popote pale ni waislam ambao siyo sunni! Huu ndio ukweli mchungu ambao wengine wasingependa usemwe wazi japo unafahamika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…