Alama "G" na "E" humaanisha nini kwenye simu pale unapotumia Data?

Alama "G" na "E" humaanisha nini kwenye simu pale unapotumia Data?

Gemini Are Forever

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2019
Posts
1,508
Reaction score
2,619
WanaJF habarini!

Mara nyingi niwapo Vijijini (sehemu ambazo network ni dhaifu) napendelea kutumia simu ndogo (ya batani/java phone) maana smartphone huwa slow kupita kiasi tofauti na simu ndogo.

Pale nikiwa kwenye data huwa inatokea alama "E" lakini kuna baadhi ya maeneo nikiwa kwenye data alama "G" hutokea japo mara chache sana.

Je, hizo alama humaanisha nini? Nini tofauti?
 
WanaJF habarini!

Mara nyingi niwapo vijijini (sehemu ambazo network ni dhaifu) napendelea kutumia simu ndogo (ya batani/java phone) maana smartphone huwa slow kupita kiasi tofauti na simu ndogo.

Pale nikiwa kwenye data huwa inatokea alama "E" lakini kuna baadhi ya maeneo nikiwa kwenye data alama "G" hutokea japo mara chache sana.

Je, hizo alama humaanisha nini? Nini tofauti?
Hiyo wanajua watengeza simu alafu acha kuongea uongo simu ya analogue kuwa picking kuliko smartphone hiyo haiwezekani
 
Mkuu Ngwango umeelewa kweli nilichoandika? Sijasema java phones zina speed kuliko smartphones, la! Nimesema java phones zina speed kwenye network dhaifu kuliko smartphone ikiwa kwenye network dhaifu (naandika/naongea kutokana na uzoefu). Ukiwa sehemu ya 2G unaweza kutumia hata dakika 30 kupakua wimbo wa 3MB kwa smartphone tofauti ukitumia java phone.

Hapa nilipo nimeshindwa kuperuz JF kwa smartphone ila kwa simu ndogo (java phone) natumia kama kawaida kama unavyoniona.
 
kinachofanya simu ndogo iwe fast na kubwa iwe slow ni browser. hio simu kubwa ukieka opera ya zamani version 7 kushuka itakuwa speed pia kwenye E ama weka uc mini version ya zamani pia 9.8 kushuka
 
Basi tu wakuchanganye mteja ila zote izo hazina speed.

1G ndio G (GPRS)
2G ndio E (EDGE)
zote G na E ni 2g, ilianza G then ikaja E ambayo wengine wanaita 2.5G.

1g ni ile network ya unaongea then ukimaliza unasema ova, mwenzako nae anaongea, ilikuwa ni 1 way tu.
 
Back
Top Bottom