Je, ni kweli alama hii kwenye kucha ni ishara ya bahati au ni tatizo ki afya?
- Tunachokijua
- Wadau wengi wamekuwa wakiamini kuwa ishara hii kwenye kucha inaweza kuashiria bahati kama vile kuokota fedha ama jambo lingine la kufanana na hilo. Lakini Je, ni upi haswa uhalisia wa ishara hiyo kwenye kucha.
JamiiCheck imefuatilia tafiti mbalimbali na makala za afya na kubaini kuwa ishara ama madoa hayo kwenye kucha mara nyingi inaweza kuashiria kwamba kucha zinapitia athari fulani.
Hali hii inaweza kutokea ama kumuathiri mtu yeyote bila kujali jinsi, umri ama asili ya mtu. Na uwepo wake inaweza kuwa ishara ya magonjwa pia. Alama hizi kitaalamu zinajulikana kama leukonychia.
Kuna aina tatu za leukonychia ambazo ni;
- Inayotokea mahali ambapo kuacha huanzia kukua/kuota na huonekana katika sehemu ngumu ya kucha (True leukonychia).
- Inayotokea kwenye ngozi iliyo chini ya kucha badala ya kwenye kucha yenyewe (Apparent leukonychia).
- Inayotokea juu ya uso wa kucha ambayo mara nyingi husababishwa na viube hai wa nje kama vile fangasi (Pseudokeukonychia).
- Jeraha kwenye kucha kutokana na kugonga kucha na kitu fulani au kubanwa kama vile na kuvaa viatu vinavyobana au kung'ata kucha.
- Mzio (Allergy) unaotokana na matumizi ya baadhi ya viambata kwenye kuccha mathalani rangi ya kucha, gel, akriliki au bidhaa za kutunza kucha.
- Maambukizi ya fangasi, ambayo yanaweza kuathiri uso wa kucha.
- Athari za baadhi ya dawa. Wakati mwingine, madoa meupe yanaweza kutokea kwenye kucha kutokana na kuathiriwa na metali nzito zenye sumu, kama vile arseniki na risasi. Pia, tiba ya saratani kwa kutumia kemikali (chemotherapy) na baadhi ya dawa zinazotumika kutibu maambukizi ya bakteria na maambukizi ya njia ya mkojo, ikiwemo dawa za sulfa (sulfonamides), zinaweza kusababisha madoa meupe kwenye kucha.
- Magonjwa fulani, ingawa si ya kawaida, yanaweza pia kusababisha mabadiliko ya rangi ya kucha. Baadhi ya magonywa hayo ni kisukari, moyo kufeli, UKIMWI, ugonjwa wa ini (cirrhosis ya ini) na ugonjwa wa ngozi (psoriasis).
- Magonjwa ya kurithi: Haya ni magonjwa au hali zinazorithishwa kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto kupitia vinasaba (genes). Vinasaba huamua sifa mbalimbali za mwili, kama vile rangi ya nywele, rangi ya macho na urefu. Baadhi ya magonjwa ya kurithi yanayoathiri kucha, kama vile Bart-Pumphrey syndrome na Darier disease, yanaweza kusababisha kutokea kwa madoa meupe kwenye kucha.