Alama ya herufi "M" kiganjani

Alama ya herufi "M" kiganjani

Omba NMungu akusaidie ,ndugu hakuna anayetajirika kwa sababu hizo
 
Mm nina M perfect kabisa
1.ni kweli nina akili sio ya kawaida kabisa
2.ni kweli ukiwa na M ni rahisi sana kupata hela ila hii ni kutokana na brain pia
3.ni kweli unavuka changamoto yoyote ambayo mtu wa kawaida anaweza kujiua
4.na ni kweli M wana bahati sana

Ila: uwe karibu na MUNGU na uepuke tu umalaya utajishangaa mno kila kitu kinaenda

View attachment 2374781
Mimi mbona yote kinyume [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hamna M hapo
20220928_145414.jpg

Hii vipi?
 
Je, wewe una alama herufi"M kiganjani? Ni asilimia 1% tu ya watu duniani walio nayo alama hiyo! Hapa ndipo unapohitaji kujua sasa maana ya alama hiyo! Tiba za kiganjani au alama za kiganjani (Palmistry) ni njia ya zamani ya kutabiri siku zijazo na tafsiri ya utu wa mtu kutoka kwenye muundo wa mistari ya mikono.

Wakati mwingine mistari hii inaweza kuunda hata nambari na herufi. Moja ya herufi hizi inaweza kuwa herufi "M" ambayo umuhimu wake umechunguzwa na wataalamu wengi. Kama wengi wanavyoamini, mistari kwenye kiganja inaonyesha tabia na hatima ya maisha yetu. Herufi "M" imepewa kwa watu maalum tu.

Wamejaaliwa ufahamu (akili) wa ajabu na inawakilisha kuwa ni washirika bora kwa biashara yoyote. Ikiwa una watu unaowapenda wana herufi "M" ndani ya kiganja cha mkono, lazima ujue ukweli kwamba huwezi kuwadhihaki na huwezi kusema uwongo au kumdanganya mtu huyo kwa njia yoyote ile. Kwa kuwa na akili nyingi na ufahamu mkubwa, watu walio na herufi "M" kwenye kiganja hugundua kwa urahisi kuwa wamedanganywa au wamepotoshwa.

Wanawake ambao wana herufi "M" kwenye kiganja wana ufahamu (akili) wenye nguvu zaidi kuliko wanaume, hata kuliko wale wenye herufi "M" pia. Wamejaaliwa uwezo wa kusimamia na kuvuka vikwazo vyovyote maishani, na kujua jinsi ya kutumia rasilimali na fursa zinazopatikana.

MAANA YA HERUFI "M" KIGANJANI KWAKO

- ustadi wa uongozi yaani kuongoza vizuri kwenye jambo lolote

- utajiri (mtiririko rahisi wa pesa)

- wenye matumaini, furaha

- fursa nzuri kumimimika

Pia ishara hii ni tabia kwa manabii. Kwa hiyo ukiwa una alama hii mkononi mwako, wewe kweli ni mtu maalum katika ulimwengu huu.

View attachment 2370789
View attachment 2370794
Mimi viganja vyangu vyote vina alama ya herufi M, kwenye swala akili na uwezo wa kupambanua mambo najikubali Mungu amenipa uwezo Mkubwa sana, huwa nawazoom Tu watu wanavyopata ugumu kuchanganua mambo tena wakati mwingine mambo mepesi kabisa, tukija kwenye swala la utajiri mmh! bado nasubiri... Lakini pamoja na yote haya mara nyingi sisadiki kwenye abstract and myth kama hizi ambazo hazina uthibitisho wa kisayansi au ushahidi wenye uliopembuka na yakinifu
17215658130958217621730779017354.jpg
 
Nairudishaje mkuu?
Usitishike ndugu hakuna cha kuibiwa nyota nadhani kuna maelezo fulani yametolewa tofauti ndio maana yanakupa mkanganyiko.
Badala ya kusema watu wenye herufi M wanakuwa na hela sana sio sahihi ila badala yake ilitakiwa aseme watu wenye herufi M huwa wana bahati,na bahati inaweza ikawa ni ya kupata pesa,kupata kazi,kupendwa na wanawake,kupendwa na jamii insyokuzunguka zote hizi ni bahati.
Na pesa haiji yenyewe bila kuwekewa mitego yaani ni lazima ujitume kwanza na kuwa mbunifu ndipo pesa ije,labda cha kujiuliza ni je kwenye kupata michongo mbalimbali ya kazi ikoje kwa upande wako?na unapambana kwa kiasi gani?hili ndilo la msingi
 
Back
Top Bottom