KWELI Alama ya jumlisha kwenye baadhi ya vidonge inaashiria kuwa kinaweza kugawanywa

KWELI Alama ya jumlisha kwenye baadhi ya vidonge inaashiria kuwa kinaweza kugawanywa

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Mdau wa JamiiCheck kutokea instagram amehitaji kujua. Je, alama ya msalaba ama jumlisha inayoonekana kwenye baadhi vidonge huwa inaashiria nini?
1764583444438.png

1764583654985.png
 
Tunachokijua
Mdau wa JamiiCheck kupitia mtandao wa Instagram alihitaji kuhua Je, ni kwa nini baadhi ya vidonge huwa na alama ya msalaba ama ya jumlisha, huwa inaashiria nini?

JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa vidonge vingi huwa na alama, nembo, namba na ishara nyingine ambazo kitaalam hujulikana kama (Pill Imprint Code).

Alama hizi mara nyngi huwa ni tofauti kulinganan na kidonge husika ama wakati mwingine zinaweza kufanana kati ya kidonge na kidonge.

Alama hizi huwekwa ili kumsaidia mtumiaji pamoja na mtaalamu wa afya anatoa dawa hizo kwa mgonjwa kujua mchanganyiko uliomo katika vidonge hivyo na mzalishaji wake.

Je, alama ya msalaba/jumlisha huashiria nini kwenye kidonge?

Baadhi ya vidonge huwa na alama ya kukatwa katikati na alama hiyo hujulikana kama "score (Pill Score)" ambayo huwa imewekwa mahusi kwenye kidonge na si urembo.

Alama hii huashiria ama humsaidia mtumiaji kujua kuwa unaweza kukivunja kidonge hicho mara mbili au mara nne kulingana na alama iliyopo.

Kwa vidonge visivyo na alama hiyo inaashiria kuwa si salama kuvigawanya. Unashauriwa pia kugawanya kidonge ikiwa umeshauriwa na mtaalamu wa afya.

Zifuatazo ni dawa ambazo hazipaswi kugawanywa nusu;
  • Dawa za uzazi wa mpango (Contraceptives)
  • Dawa za matibabu ya saratani (Chemotherapy medications)
  • Dawa za mchanganyiko ambazo zina viambato zaidi ya kimoja hai (Combination medications that contain more than one active ingredient)
  • Dawa za kuzuia damu kuganda (Blood thinners/Anticoagulants)
  • Dawa za kuzuia kifafa (Anti-seizure medications/Anticonvulsants)

Tahadhari muhimu: Kamwe usigawanye dawa bila kuuliza mfamasia au daktari kwanza, hata kama zina mstari wa katikati. Baadhi ya dawa zikigawanywa zinaweza kuwa hatari au kupoteza ufanisi.
Back
Top Bottom