Alama za mnafiki

Alama za mnafiki

bagwell

Senior Member
Joined
Sep 19, 2012
Posts
113
Reaction score
25
Alama za wanafiki, ni tatu bora uzijue
Katu nae haaminiki, japo ahadi azitoe
Pia na hasadikiki, hatumizi maaganoe

Alama yake ya pili, mnafiki ni mrongo
Maisha hana ukweli, wala mizuri mipango
Yake usiyakubali, atakukoroga bongo

Akiaminiwa hukhini, mnafiki ni sifaze
Hachi na hana dini, hudhulume nduguze
Usimtie nyumbani, na sirizo simjuze
 
huyo ni vasco! ujumbe umfikie popote alipo, ye na mafisadi wenzie pamoja na rizmoko, laanakhum!
 
Si bora uwataje japo kwa majina tuwajue!
Waloahidi meli mpya kwenda Bukoba;
Wakaahidi bwawa la kufuga samaki umasaini,
Maisha bora kwa kila mtanzania,
Hari mpya, kasi mpya (kumbe kasi ya wizi tu)

Angalizo: Lizmoko kwenye maandiko ni Malaika aliyeko peponi anayetoa dhawabu za ajabu kwa wale wamchao bwana wa lizmoko! Linganisha na Lizmoko wa Bongo!
 
Back
Top Bottom