enzo1988
JF-Expert Member
- May 26, 2018
- 1,838
- 7,346
Hizi ni alama kuu ambazo hupatikana katika majengo ya kufanyia ibada takatifu katika dini ya Kiislamu ambayo hujulikana kama msikiti(misikiti).Alama hizi ni mwezi mpevu pamoja na nyota.
Historia yake:
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya kihistoria, hizi alama zilianza kutumika kuanzia karne ya kumi na tano na hii ni baada ya dola ya Ottoman kuishinda dola ya Byzantine (Himaya ya kirumi ya Ugiriki) na hatimaye kuliteka makao makuu ya jiji lao kuu yaliyojulikana kama Constantinople (Instabul kwa sasa).
Hizi alama za mwezi mpevu na nyota zilikuwa zikitumika na himaya ya Byzantine, hivyo wa Ottoman walizichukua na kuziongezea pamoja na kuzitumia katika maeneo mbalimbali.
Katika kujiongezea maeneo, Ottoman waliendelea kuvamia maeneo mbalimbali hasa Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini ambako imani ya dini ya Kiislamu ilikuwa tayari imeota mizizi.
Himaya ya Ottoman ilifanikiwa kuwashinda wenyeji wa maeneo haya na hivyo ilifanikiwa kuyakalia na kuyatawala maeneo haya kwa muda mrefu.
Maswali: (Kwa wanazuoni ,wajuzi na wabobevu wa dini ya kiislamu)
Nb 2.Nia ni kujifunza na kuelekazana na siyo kubishana.
Nb 3.Samahani kwa wote ambao watakuwa wamekereka.

- Je, uwepo wake ni sahihi??
- Kama siyo sahihi kwa nini haziondolewi???
- Zilikuwepo wakati wa Mtume???
- Kwanini hazikuwepo wakati wa Mtume ????
- Quran inaelezeaje juu ya uwepo wa hizi alama?