Dr Count Capone
JF-Expert Member
- Feb 7, 2017
- 1,878
- 3,263
-----------------IN FACT----------------------
UNAFAHAMU KUWA URUSI ILIIUZIA MAREKANI JIMBO LA ALASKA?
ALASKA ni jimbo lililopo kaskazini-magharibi mwa bara la AMERIKA KASKAZINI,kwa upande wa mashariki jimbo hili limepakana na BRITISH COLUMBIA na YUKON ambayo ni maeneo yaliyo chini ya mamlaka ya nchi ya CANADA,kwa upande wa magharibi ALASKA imepakana na bahari ya CHUKCHI kwa upande wa kusini na kusini-magharibi imepakana na bahari ya PACIFIC,KASKAZINI imepakana na bahari ya ARCTIC .Pia miliki ya bahari ya ALASKA inakaribiana kabisa na miliki ya bahari ya URUSI ikiwa kuna umbali wa MAILI TATU tu zinazotenganisha hizi miliki mbili.
MUST-READ: KAMA BADO HUJA'LIKE' PAGE YETU YA FACEBOOK IITWAYO "CLYZ MOOD" LIKE HIVI SASA KUPATA FACTS NYINGI KAMA HIZI,PIA WAAMBIE MARAFIKI WA'LIKE', PIA USISITE KUTUACHIA MAONI YAKO HAPA CHINI
UKOLONI WA URUSI NDANI YA ALASKA (KWA UFUPI)
ALASKA iligunduliwa na watu kutoka ULAYA mwaka 1741,ambapo URUSI ilikuwa ikitanua maeneo ya miliki yake,moja ya watu waliokuwa wakisaidia katika kugundua maeneo mapya ni nahodha kutoka DENMARK bwana VITUS BERING ambae alitokea kuona eneo la ALASKA mwaka 1741.
KOLONI la mwanzo la URUSI ndani ya ALASKA ni eneo lililopewa jina la THREE SAINTS BAY linalopatikana katika kisiwa kiitwacho KODIAK ISLAND,eneo hili lilifanywa koloni mwaka 1784.Mawasiliano ya mwanzo kati ya waamerika wa mwanzo na warusi yalikuwa ni ya kibiashara
Mfanyabiashara wa manyoya kutoka URUSI bwana SHELIKOV aliishi THREE SAINTS BAY katika kisiwa cha KODIAC yeye na mkewe pamoja na wafanyakazi wake wapatao 200 kwa miaka miwili,wakati akiwa kisiwani hapa aliendelea kulitazama kwa karibu eneo la bara la ALASKA kwa kutumia wapelelezi wake waliokuwa na kazi ya kulipeleleza ili kujua fursa za kibiashara zinazopatikana eneo la bara(ALASKA),walifanikiwa kutambua fursa zilizokuwa zikipatikana katika eneo la bara la ALASKA na vituo vipya vya biashara ya manyoya viliweza kujengwa.Mwaka 1786 bwana SHELIKOV alirudi URUSI na mwaka 1790 alimchagua bwana ALEKSANDR BARANOV kusimamia shughuli zake za kibiashara ndani ya ALASKA.
Bwana BARANOV alianzisha kampuni iitwayo RUSSIA AMERICAN COMPANY iliokuwa ikijihusisha na biashara ya manyoya na kufanikiwa kuiendeleza kampuni hiyo kwa kiwango kikubwa na kufikia maeneo ya AMERIKA KASKAZINI, mwaka 1812 alifanikiwa kuanzisha makazi ya warusi huko CALIFORNIA KASKAZINI lakini migogoro kati ya URUSI na WAINGEREZA ilipelekea URUSI kuachia maeneo ya AMERIKA KASKAZINI na hivyo kubaki na LASKA pekee.
Katika miaka ya 1850 vita vya CRIMEA viliisababishia URUSI hasara kubwa hivyo kukosa fedha za kuendeleza baadhi ya makoloni yake kama ALASKA.
UUZWAJI WA JIMBO LA ALASKA
Jimbo hili liliuzwa kwa marekani kutoka kwa URUSI (RUSSIAN EMPIRE) kwa mkataba uliosainiwa MACHI 30, 1867,mkataba ulisainiwa na katibu wa nchi wa wakati huo William Seward na waziri wa urusi kwa marekani Edouard de Stoeckl.
RUSSIAN EMPIRE iliuza ALASKA kwa thamani ya dola za kimarekani milioni 7.2 ambapo kwa sasa ni thamani sawa na dola za kimarekani milion 123.
KWANINI URUSI (RUSSIAN EMPIRE) ILIUZA ENEO LAKE LA ALASKA?
Hili ni moja ya swali lililoulizwa na mwanachama mmoja wa mtandao wa QUORA.COM ambapo mwanachama huyo aliuliza ni kwanini RUSSIAN EMPIRE (URUSI) iliuza eneo ALASKA lake kwa MAREKANI?.
Miongoni mwa sababu zinazotajwa kuwa zilichangia RUSSIAN EMPIRE kuiuza ALASKA kwa MAREKANI ni hizi.
>URUSI (RUSSIAN EMPIRE) ilikuwa kwenye hali ngumu ya kifedha hivyo EMPEROR ALEXANDER II alihofia kupoteza eneo lake hilo kiwepesi katika vita yeyote ambayo ingezuka.
>ALASKA au RUSSIAN AMERICA ilkuwa karibu na eneo la BRITISH COLUMBIA lililokuwa likimilikiwa na BRITISH (WAINGEREZA) EMPEROR ALEXANDER II alihofia kulipoteza eneo hilo kwa mahasimu wao wakubwa WAINGEREZA(BRITISH) na pengine alitumaini kuliuza kwake kwa MAREKANI kungezua migongano kati ya MAREKANI na UINGEREZA ambao nao walikuwa mahasimu.
>Kutokana na hali ya kifedha ya RUSSIAN EMPIRE,URUSI iliona kuwa kama kungezuka vita nyingine maeneo ambayo kwao ilikua ngumu kuyalinda yangekuwa ndio 'Target' kubwa kwa mahasimu wao.Vile vile ALASKA kwa wakati huo haikuwa yenye faida kubwa kwa URUSI (RUSSIAN EMPIRE) hivyo EMPEROR ALEXANDER II aliona kuliuza eneo hilo kuna faida kuliko kuendelea kubaki nalo.
Na baadhi ya maswali mengine yanayoulizwa sana na watu ni
je,URUSI itahitaji eneo lake la ALASKA tena? na kama ndio
je, wako tayari kulitwaa kivita au kulinunua kama walivyouza?
Na je, marekani watakubali kuliachia eneo lao hilo?
Na ikumbukwe kuwa ALASKA haijapakana na eneo lolote la MAREKANI(kama picha hapo chini inavyoonesha)
FAST FACTS.
>ALASKA NI JIMBO KUBWA ZAIDI MAREKANI LIKIWA NA UKUBWA WA (1,717,856 km2,NA PIA NI MOJA YA MAENEO YALIYO WA IDADI NDOGO YA WATU IKIWA NA MAKADIRIO YA WATU 741,894 (kwa mujibu wa sensa iliofanyika mwaka 2016.)
>ALASKA NI JIMBO LILILO NA UWANDA MREFU ZAIDI WA PWANI KULINGANISHA NA JIMBO LINGINE LOLOTE LA MAREKANI.
>JIMBO LA BRITISH COLUMBIA limeitenganisha ALASKA na WASHINGTON kwa maili zipatazo 500 (km 800).
>hakuna barabara inayounganisha eneo la JUNEAU (mji mkuu wa ALASKA) na maeneo mengine ya AMERIKA KASKAZINI.
>ALASKA ni kubwa mara mbili ya jimbo la TEXAS ambalo ni la pili kwa ukubwa.
>Ndani ya ALASKA kunapatikana mlima wenye kilele kirefu zaidi barani AMERIKA KASKAZINI ambao ni mlima DENALI.
>kulingana na ripoti ya OCKTOBA 1998 mamlaka ya ardhi ya marekani ilionesha kuwa aslimia 65% ya ardhi ndani ya ALASKA inamilikiwa na serikali.
>Gharama za kuendesha maisha ndani ya ALASKA zinatajwa kuwa ni za juu kuliko maeneo mengine ya MAREKANI,maeneo haya ni hasa ya vijijini ambapo ufikaji wa bidhaa muhimu kwa njia ya usafirishaji imekuwa ni ngumu kutokana na miundombinu.
PROUDLY
#SPONSORED_BY
JSRindustries
CLYZ MOOD FB PAGE
IN ASSOCIATION WITH
KENDRICK STUDIO