Alaumiwe nani kati ya tcu, jeshi na serikali? Aibu ya nani

Alaumiwe nani kati ya tcu, jeshi na serikali? Aibu ya nani

Joined
Aug 28, 2013
Posts
33
Reaction score
4
Mimi naona wote wanamakosa, hivi TCU hawakuona kwamba JKT wamesema AWAMU YA 3 ni mwezi huu wa 9? na je JKT hawakuona na tena walitangaza hadi walitangaza mpaka redioni vyuo vinafungua na waziri ameaprove kama waliona kuna makosa y wasingekaa nyuma ya pazia na kujadiliana kwa kina na kukubaliana, hata kama jeshi wanasheria lakini wanatakiwa wajue nao wapo chini ya katiba ya TZ so na wengine wanahaki pia hivyo wasifanye mambo watakavyo, jambo walilolifanya limeonyesha udhaifu kwa jeshi, TCU, serikali na vijana hata kama wataenda watakwenda na kinyongo hivyo hato huo uzalendo wataofuzwa utakuwa hauna faida hatatone na pia hii itafanya vijana waone na kudharau jeshi hivyo hata migomo chuo itatokea tu kutokana na kwamba vijana kupewa mafunzo wakiwa na kinyongo na pia kudharau jeshi, kiukweli jeshi wamejishushia heshima pamoja na serikali, na nadhani itakuwa ni busara na hekima endapo kawambwa na naibu wake wakijiuzulu kuonyesha uwajibikaji wao maana waziri wa ulinzi na waziri wa elimu wanawasiliana y leo wote watofautiane? inamaana kuna makundi katika baraza la mawaziri. Hapa ndipo wanaanza kuwafanya vijana waone wote hawafai na ule usemi wa mapinduzi huletwa na vijana naona unaelekea kutimia, muda ukifika serikali itajutia maamuzi na vioja vyake
 
Tena usirudie kulaumu jeshi langu...jesh kazi yake ni kutekeleza tamko la serikali.so ilaumu serikali yako..OVER
 
Ndio raha ya kuwa na serikali ya kila mtu ni msemaji na kila mtu (idara) ina maamuzi....no matter what
 
Hii itakuwa ni operesheni kimbunga imeingia kwenye sekta ya elimu nahaya ndiyo matunda ya kuiwa na serikali inayoendeshwa kwa mtazamo wa vimbunga! Kazi tunayo watanzania
 
Wakati nilipofiwa na mtoto wangu kwa ajili ya mateso aliyoyapata huko msange jkt tabora kuna jamaa mmoja alinifariji na kuniambia kwamba nchi yetu mi kama dimbwi la kambare au shimo la panya kila mtu ana sharubu.jkt imeanzishwa mithili ya zimamoto bila ya kujali ratiba kama hizo zilizotajwa hapo juu.jkt imeanzishwa na bajeti finyu,miundo mbinu mibovu,mazingira hatarishi.waalimu au maafande wa kozi hiyo ya miezi mitatu na ya pekee duniani ni form 4 failures na std 7 drop outs ambao wanasubiri kwa hamu kuwasulubu f6.matokeo ya matatizo yote hayo ni vifo kwa vijana hawa wa f6 ambao walitarajiwa kujiunga na vyuo.ktk msgs mbali mbali hata humu kwenye mitandao yetu kuna tuhuma za maafande kulazisha ngono na mabinti wa f6 na kuwaambukiza ukimwi.kwa mantiki hiyo jkt ni kulaumiwa kwa kila hali kwani imeanzishwa sio kwa kuwafunza vijana uzalendo bali kuharibu maisha yao.pamoja na mapungufu makubwa ya jkt ikiwa ni pamoja na mauaji ya vijana inashangaza kuona wakubwa jeshi hilo wanavyojinadi kwenye vyombo vya habari.lkn wahenga walisema vibaya vyajitembeza na vizuri........Malizia mwenyewe
 
Back
Top Bottom