Albert Chalamila akiandaliwa vizuri, anaweza kuwa Katibu wa Uenezi mzuri sana wa CCM. Anahitaji mentorship kumuondolea mambo madogo madogo yanayomkwaza kiuongozi.
CCM inaweza kumuweka karibu na magwiji ya Siasa yakaendelea "kumpika", na pia akapata mafunzo ndani na nje ya nchi, hasa katika vyuo bingwa vya masuala ya Siasa na propaganda.
CCM irudie utaratibu wa kuchukua wanachama wake, kiwapeleke mafunzo ndani na nje ya nchi kwa malengo maalum. Kila mwaka wakipeleka vijana 10-20, wanatosha.
Pia Katibu Mkuu anapofanya ziara mikoani, awe anaibua vipaji ngazi za chini, anawapandisha juu. Ndio maana nilimshauri Kila anapofanya ziara, asiache kuongea na jumuia ya vijana ya wilaya anayopita, awape fursa ya kuongea, achuje vipaji. Mambo ya kupita mabarabarani unahutubia unaondoka, sidhani kama Yana tija, au kukaa katika mkutano wa hadhara ambao una watu maalum wa kuongea.
Kwa pale CCM angalau chalamila anafaa kuwa rais maana yake anakubalika na rika zote na Hana kashfa ya ufisadi na pia ni mtenda kazi sio porojo na mpambanaji pia hayegemei kubebwa kama wale watoto pendwa