Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema haridhishwi na kasi ya ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka ya Gongo la Mboto na kama hali itaendelea hivyo atamuweka ndani mkandarasi au mhandisi mshauri.
Ametoa kauli hiyo leo Aprili 18, 2024 alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa barabara ya awamu ya tatu ya mradi wa mabasi yaendayo haraka yenye urefu wa kilomita 23.6 inayojengwa kati ya Gongo la Mboto hadi Katikati ya mji chini ya mkandarasi Syno Hydro.
Chalamila amefanya ziara baada ya kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa wakazi wa eneo hilo juu ya tabu wanayoipata kufuatia ubovu wa barabara uliosababishwa na ujenzi unaoendelea.
Chalamila amesema mara zote mkandarasi amekuwa akijinasibu kufanya kazi usiku na mchana lakini hakuwahi kumshuhudia.