Albert Chalamila atishia kumuweka ndani mkandarasi wa Mwendokasi

Huyo Chamalila haoni mvua zinazoendelea, ujenzi unaenda vipi kwa speed kubwa na mvua hizi.
 
mkataba umesema akichelewa atiwe ndani ? acha mikwara mbuzi wewe Chalamila!

hawezi kufungwa mtu hapo, na akikamatwa kesho anatoka....

kama kidume enforce the contract! ...mkate malipo, dai specific performance, au sitisha ukandarasi, weka mwingine kupitia mahakama....

bungeni wana hati za dharura, na mahakamani emergency docket zipo, kesi ipelekwe moto chini kwa manufaa ya umma, hatima ya ujenzi na mkandarasi inaeleweka ndani ya wiki....

Tunaongozwa na watu incompetent, hawana uwezo wa ku administer mambo ya nchi, na tukishajua hawana uwezo hatuna nguvu ya kuwatimua... hili ni tatizo moja kubwa la dunia ya tatu
 
Hayo mamlaka ya kuweka watu ndani kiholela kapewa na sheria gani? Ifike mahali wanaowekwa ndani wawafungulie madai mahakamani. Kitu pekee kinachoruhusiwa na sheria Mkuu wa mkoa/wilaya ni pale Mtu anapofanya kosa la jinai mbele yake au kusababisha uvunjifu wa Amani.
 
Ila kwa tabu wanayo pata watu wa Gongo la mboto ni kama kuzimu!

Yani kuanzia pale tazara hadi gongo la mboto ni matope tupu na mashimo.

Ukitoka hapo njoo majohe na ukonga yote barabara hazifai hadi za mitaani.

Hakuna jimbo la kipumbavu kama la ukonga.

Tuna mbunge zoba sana, yuko busy eti mgogoro ya ardhi huku jimbo liko kama choo
 
Huyu naye na kichwa chake kama tunguli ana mikwala mbuzi
 
Hawa wanasiasa wapiga domo mkandarasi yuko na mkataba ndani ya mkataba kila kitu kimeelezwa tena kwa vifungu vya sheria mpaka ucheleweshaji na namna mkandarasi atakavyo adhibiwa (LD- Liquidated Damage) anapotokea mwanasiasa anapiga domo bila kuangalia mkataba unasema nini ni kama anatafuta umaarufu wa bei rahisi au asikike na yeye yupo.
 
Mikataba yote ya miradi kama hiyo huwa na utaratibu wa namna ya kushughukilia linapotokea tatizo la namna hiyo.
Siyo kumuwela mahabusu Afisa wa Kampuni.
 
Huu uchafu wa mwendokasi Bado wanaujenga wa Nini?ilivyo na huduma mbovu Hivyo Bado wanaendelea tu kujenga.Ni Bora mjikite kupanua barabara lakini siyo hiyo takataka inayoitwa mwendokinyonga
 
Nchi imejaa viongozi vichaa watupu, unamuwekaje ndani mchina aliyekupa mkopo wa kujenga hiyo miundombinu?
Pesa inatoka china, mkandarasi katoka china, kwa ufupi mchina anatusaidia! Sasa unamuwekaje ndani mkandarasi wake? Siasa za kipuuzi hizi!
Hii ni sawa, na mtu anakudai bilioni kumi, harafu unatishia kumuweka ndani mtoto wake kisa kagoma kukulipa buku ya bodaboda!
 
Hao Sino contract si ni hao wachina kila mahali wana malalamiko.
Mbona wapo tu mtaani?
Funga hao panya wapotee kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…