Albert Chalamila: Kizazi ambacho kimepata divisheni 0 au 4 tunakiweka kwenye kundi lipi? Tunazalisha kizazi ambacho hakina tija kwa taifa

Kwenye chama chetu wapo wengi wa namna hiyo je anawazungumziaje hao? Tuanzie hapo kwanza
 
Kila binadamu ni asset, hizo 0 na 4 zimejaa huko huko kwenye chama chake, yeye mwenyewe aonyeshe cheti chake cha form 4 kama Hana 4 ya mwisho
 
Hawa ndo baadae utawakuta ni mafundi, wakulima, wamiliki wa malori, wenye ma guest house na bar, daladala za usafiri na wengine wanasiasa.
Huwa wanarudi kupata elimu ya mtaa kwa vitendo, wanaanzia chini kabisa.

Wa kuonewa huruma ni hawa wenye dv 1, 2 na 3 kisha baada ya kumaliza chuo wanakosa ajira. Hawa kuwaambia rudi anza moja kama yule aliyepata 4 na 0 ni kuwadhalilisha.
 
Sidhani wala siamini waliopata Div. 0 na 4 kua hawana akili. Wakurugenzi wengi wa sector binafsi Aidha hawajaenda shule kabisa au ni la saba au wameishia kupata sifuri form four.
Wakurugenzi (executives) wengi wamesoma labda kama unasema wakurugenzi wa saluni za kunyolea. Ambao wengine hawajasoma ni founders.
Nchi kama china wanaangalia pia na uwezo wa mtu umelalia kwenye fani gani na anapelekwa huko hata kama ana sifuri. Kila mtu ameletwa duniani kwa kusudi lake.
China utaratibu wao wa kuingia chuo ni kwa kufaulu high school tu, mwanafunzi afaulu mtihani wa Gaokao ndio aingie chuo kikuu hakuna namna nyingine. Hata uwe bondia au mwanariadha kiasi gani, hujafaulu mtihani huendi chuo. Na China ina wanariadha wengi wenye fani zao wametoka vyuoni, elimu haizuii mtu kuwa na kipaji.

Hata sisi ni hivyo, hakuna mtu anakatazwa kuwa bondia au mchezaji ila usitake kufanya kufeli sekondari liwe jambo la kujivunia.
Mkuu hajadharau waliopata sifuri. Kama kupata sifuri ni jambo jema tungekuwa tunahimizana kugonga miswaki na kuzungusha kwenye mitihani.

Sio jambo zuri wengine wanafaulu, wengine wanagonga sufuria kabisa lazima mikakati ifanywe angalau hii elimu ya sekondari mtoto apate marks kidogo za kumuendeleza fani au kipaji chake kwa elimu. Awe na options sio alazimike kuimba singeli.
Majeshini wengi ni Darasa la saba na Division 4 na ziro na vyeti vya kufoji lakini unakuta mtu anakusetia Mzinga kwa mahesabu ya hali ya juu sana hata msomi wa chuo kikuu hawezi.
Hao Div 4 na Zero wanaseti hiyo mizinga bila training? Na hao wasomi wa chuo kuna kozi ya mizinga walipelekwa wakafeli?

Au ndio unalinganisha mradi huyu ana Degree basi anatakiwa ajue kila kitu hata kama kinahitaji mafunzo na uzoefu wake. Ingekuwa hivyo basi kila graduate automatically angejua kuendesha bodaboda na malori.

Mkuh hata wewe wanao huwezi washawishi wafeli, tuwe wakweli hapa tusitiane moyo.
 
Nyie wenyewe mnazalisha wakata mauno...na ujing ujing uchawa
Upuz ndy mnaupa kipaumbele
Mpaka sasa mshazalisha takataka za kutosha
Na bado huko mbeleni mambo yatazidi kuwa mabaya

Ova
 
Kwann mnapenda kuandikamo viingereza, muandike luga ya taifa?
 
Mbona bungeni kuna ambao hata hawajapata hizo zero na four?
 
Hakuna mtu anayebeza elimu, lakini si haki wanaojifanya wana elimu kuwabeza wasiyobahatika kuhesabiwa ni wenye elimu kisa tu kuwatahini wanafunzi kwa yale ambayo wenye elimu wanadhani kuwa nayo ndiyo kuwa una elimu. Watanzania tunajijua wenyewe kutokana na roho zetu mbovu tunatumia juhudi kubwa katika kukwamishana kimaisha kuliko kusaidiana kufanikiwa. Na wanasiasa kila jambo wanalichukulia kisiasa.
 
Kwanza nikupongeze nakukusifu kwakutumia mda wako mwingi kudadavua hii message yangu mimi sikushabikia ziro. Ila nimezungumzia ni kwanini Ziro zinakuwa nyingi kwenye shule za kata.
 
Kuna watu wengine ni kama vile akili hawanaga! Au ni akili fupi kama mkia wa mbuzi,
mtu anaepata zero au four kidato cha nne sindio hawahawa wako kwenye majeshi yetu? Sindio hawahawa ni wajasiriamali mnawakata kodi kila mwaka?
Umewai kumkuta mtu aliepata four amekaa tu analishwa na kutunzwa?

Kizazi hakina tija kwa taifa na mbona mnawakata kodi kwenye biashara zao?
Wewe Chalamila unaichangia hii nchi kodi kiasi gani?


Upumbavu na elini za kikoloni bado zimejaa vichwani mwa watu
 
Naomba niulize Wafanya biashara wote pale Kariakoo wote wana Div One na Two?
 
Kwanza nikupongeze nakukusifu kwakutumia mda wako mwingi kudadavua hii message yangu mimi sikushabikia ziro. Ila nimezungumzia ni kwanini Ziro zinakuwa nyingi kwenye shule za kata.
Kuna mkono wa serikali hapo kwa shule hizo kupata ufauru mbaya. Mfano haiingii akilini ni vipi watoto wote 45 waliomaliza darasa la saba shule X ya Private na kupata alama A masomo yote wakapelekwa wote kama walivyo 45 shule Y ya sekondari ya kata iliyo jirani na walipomalizia la saba. Then utegemee ushindani wa kimasomo hapo 😎
 
Sasa kodi zetu zinatumika kwenye mambo ya anasa za kipuuzi kama kuwalea wateule na kusahau kabisa kuwekeza kwenye huduma za elimu na afya lazima shule na vyuo viendelee kuzalisha matutusa na mwishowe wanaishia kuwa chawa na mashoga tu
Kwa nini uzae wakati hali yako mbaya ? Inabidi tuishi kadri ya uwezo wetu. Unambato bila kondomu wakati uhakika wa kula milo mitatu kila siku hauna. Je mtoto na mama yake utaweza kuhudumia. Inabidi tuamke aisee.
 
Mimi ni miongoni mwa zero ila nmewazidi maarifa watu wengi sana wenye degree.. ajifunze kuchanganua
Elimu iliyopo ni ya hovyo kupata kutokea
 
Binaadamu yoyote ktk dunia anatija.
Kupata div 1 au 2 sio kwamba umeibuka kimaisha.
Kwaio mkuu una bishana na mteule wa mama Samia mwenyekiti CCM taifa..

Division 0 na four hazina tija kwa dunia ya Sasa ni Bora mtu aende veta miaka minne kuliko secondary school Tena apate division zero au four ya mwisho mwisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…