GE2025 Albert Chalamila: Nimesoma mitandaoni kuhusu fujo Oktoba 29, ndugu zangu mji wenu uko salama

GE2025 Albert Chalamila: Nimesoma mitandaoni kuhusu fujo Oktoba 29, ndugu zangu mji wenu uko salama

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema kumekuwepo na baadhi ya maandiko mbalimbali mtandaoni kuwa Vijana na Makada wa Vyama vya siasa wanahamasisha maandamano siku ya Uchaguzi Mkuu Octoba 29, 2025 ambapo amewaonya wanaotaka kujaribu kufanya vitendo hivyo kwani hawatofanikiwa.

Chalamila ameyasema hayo hii leo Octoba 15, 2025 wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Barabara ya Kongowe hadi Mbagala ambapo Chalamila amewatoa hofu Wananchi wa Dar es Salaam na amesisitiza kuwa Mkoa uko salama huku akisisitiza ugomvi wa Vyama vya siasa usivuruge amani kwani Nchi itaendelea kuwepo hata baada ya uchaguzi.

“Nimesoma kwenye mitandao ya kijamii kuna baadhi ya Vijana wenzetu, Makada wa Vyama vya siasa wanasema tarehe 29/10 siku ya uchaguzi wataandamana, watafanya fujo wengine wamesema sijui watakwenda kuchoma vituo vya mafuta mimi naomba niwaeleze ndugu zangu wana kongowe mji wenu huu wa Dar es Salaam uko salama sana usije kuogopa hata wewe unataka kufanya hivyo usiogope we nenda kajaribu kufanya unachotaka kufanya nakudhibitishia kabla ya kupeleka mguu wako mbele utakuwa umesha Sali baba yetu zaidi ya tano”

....Umesoma Mtandao Gani kuhufu fujo, ili nasi tukasome? Maana Mitandao yote inasema ' Maandamano ya AMANI ! 😏😏
 
Back
Top Bottom