BabaMorgan
JF-Expert Member
- Dec 18, 2017
- 4,869
- 13,137
Albert Mangwair
Kupitia mahojiano aliyofanya Skywalker Fredrick Bundala na Makaveli aliyekuwa mmiliki wa ghetto ambalo msanii mkali wa freestyle Ngwair akiishi amefunguka mengi kuhusiana na nyakati alizoishi na Ngwair kubwa zaidi ni lifestyle ya msanii.
Anafunguka Ngwair kuwa mtu wa Bata ambaye anaweza kupata millioni Moja au mbili jioni ila kesho asubuhi akaamka ana kitu means hela yote imeisha kwenye kumbi za starehe mwendo wa kuchange location till morning.
Licha ya kuwa na wimbo unaozungumzia geto kitu ambacho kilutuinspire vijana wengi kutamani kumiliki magheto makali kitu cha ajabu Ngwair hakuwa na ghetto hilo analozungumzia bali alikuwa akiishi kwa Makaveli.
Makaveli anaendelea kuwa Ngwair alianza kumiliki gari kabla ya ghetto na alikuwa akitembea na nguo kwenye buti popote pale usiku utakapomkuta basi ndio hapohapo atakapoangusha.
Ni maisha ya aina gani kwa kijana ambaye unafame na unapata pesa kukosa sehemu ya kupaita kwako washikaji wanaweza kukupenda Kila mtu akawa anatamani uwe naye karibu kwa sababu una kipaji au unawafurahisha lakini washikaji haohao behind your back wanakushangaa na kukuona ni hopeless how come ushindwe kupanga hata room master ila batani unateketeza Hadi millioni.
PIA SOMA
- No Agenda: Maisha ya Ngwair alijiona New York akiwa Bongoland