#Maskini wenzangu:
* Wachache ndio wanaishi, wengi wetu maEscort
Twiga wanapanda pipa hata bila ya passports
Mikoa mingi bado haina hata airports
Zaidi ya migodini madini kuyaExport.
* Bila ya wazawa kufaidika
Ndio maana waZanzibara wamechoka kutanga na Tanga na Nyika
Big up Mandela leo South sio Afrika
Waliotangulia kupata Uhuru bado wanapigika
Bidhaa zilizoExpire hutubambika
Meli zinazidi zama wengi Daily tunawazika
Wenye hali duni ndio tunaoathirika
Wao maBig Sound Special Order, uhakika.
* Tutalia machozi ya damu mpaka yatafumba ardi
Na tutaogelea wenyewe na watu hawatojali
Lete mgomo baridi uijue Serikali
Then umuulize Ulimboka umuhimu wa Madaktari.
* Viongozi wa siasa kama viongozi wa dini
Mengi wanaongea 'coz silaha yao ni ulimi
Mh. Spika, Tanzania, Uhuru inazidi zeeka, tayari ni miaka hamsini.
* Mengi mmetuahidi pia ahadi ni deni
Pia tunatambua umuhimu wa UN
Kupinga HIV, Umasikini na Rushwa, and
Mabilioni yanayotumika kwa Campaign
* Kama zakupinga unyanyasaji wa watoto
Zisiishie kwenye Promo na kuwalisha bado ndoto
* Issue sio kutupiana maneno bungeni
Bali watoto watoke mtaani, warudi shuleni
Mkulima shambani anahitaji usafiri wa treni
Nyie piteni angani, mazao yake muuzieni
* Mpeni bei nzuri, hawezi mudu zaidi ya trekta
Ni mawazo tu DIK usione na kuTETA.
'MASIKINI WENZANGU'
* TANU ilifanya kazi kubwa sixty one
Solution sio rada, Nchi kuichukuwa upinzani
Bali Mtanzania wa chini anaishi maisha gani
Watu wanakufa kwa njaa, iweje tujivunie amani
* Mengi tu mazuri yamefanyika mpaka sasa, ila naamani bado tungekuwa mbali
* Hivi Babu wa Loliondo nayo inawezekana tu ilikuwa ni siasa, NO!, Lakini iko wapi kaburi ya Balali
* Men, jibu unalo so usiulize swali
Unadini ! Mkristo sali na Muislam swali
'coz
* Bado tunaishi ki Mungu Mungu
Kwenye M weka Z usikie kizunguzungu
* Jinsi Ukoloni unavyofanya Mambo mpaka leo
Kuongoza jamii sio kumtawala mkeo
* Najiuliza maisha yangekuaje bila muziki
Hivi mtaani ingekuwa vipi !?
INGEKUWA MZIIIKI.