Albert Mangwair alifahamika zaidi kwa jina la Ngwair, alifariki takribani miaka 7 iliyopita huko Afrika Kusini alipokuwa kwa shughuli zake. Alitamba kwa vibao vikali kama ‘She got gwan’ ‘gheto langu’ na ‘Mikasi’
Alikuwa ni mmoja wasanii katika kundi la Chamber Squad akiwa yeye, Dark Master, Mez B (Marehemu pia) na Noorah
Marehemu Ngwair alikuwa amepata umaarufu mkubwa katika ulimwengu wa hiphop kutokana na uwezo wa kufanya mitindo huru, ‘free styles’ na ndipo alijiita cow-weezy, kwa kujifananisha mitambao ‘styles’ na Lil Wyne, aliyekuwa anajiita Lil Weezy
Leo ni kumbukumbu ya kifo chake, Je wewe unamkumbuka Mangwair kwa jambo lipi, Mstari upi wa #Ngwair unaukumbuka, Wimbo upi uliupenda