Albert Mangwea (Special Thread)

Albert Mangwea (Special Thread)

Gwair na Chid Benz walikuwa na kiwango cha kufanya battle ya freestyle na kina Big T,Busta, Jadakiss ama Cassidy
 
But still yuko around mazee.. Kazi alizoacha zinaishi, na kingine kizuri P funk aliwahi kusema ana track za Mangewear ambazo bado azijawa release... Uenda akaja ziachia!
 
She got a gwan,bado nimo,mademu wangu,zawadi na nyingne nyingi katika albamu yake ya a.k.a mimi alivunja si kitoto. Ndo msanii wangu bora wa muda wote na ndo ilikua mara yangu ya kwanza kununua album ya msanii wa kibongo
 
~~ Huyu jamaa alikuwa unaweza kurap na kuimba pia...alifuata ni marehem pia king zilla....ndio wanakuja hawa vizazi vingine,Hawa jamaa wangeshiriki kwenye dakika 10 za maangamizi sijui wangeuaje?
 
ngoma hadi leo naipenda ni dakika moja!huwa inanipa feelings flan amazing sana
 
Ngwair atabaki kuwa msanii bora aliyebadili hiphop/rap kuwa commercial na hardcore. Alitambulisha Hadji ya freestyle ambayo bado hajapatikana wa kuziba pengo. Wanatapatapa tuu
 
Yani leo nimeisikiliza "Mikasi"nikakumbuka way back life la school boarding tunapoenda disco wakipiga huo dah ilikua shangwe sana. Yani ni mziki mkali wa all tym RIP Albert
 
" Ngwair mbona huonekani? ,vipi hauna tv?Ungekuwa na faida nami ungeniona kwa 3d.
 
120 kwenye kona Shaaaaa!!! Hata nikifa leo pengo langu halina spare so nageuka mac regan nawaambia "ENDELEAAAA".

Hapa watoto wadogo hawamjui hata Mac Regan ni nani na Endelea ni nini 😀😀😀.
 
120 kwenye kona Shaaaaa!!! Hata nikifa leo pengo langu halina spare so nageuka mac regan nawaambia "ENDELEAAAA".

Hapa watoto wadogo hawamjui hata Mac Regan ni nani na Endelea ni nini 😀😀😀.
Nifafanulie kidogo mkuu kuhusu Mac Regan na Endeleaaa
 
Marehemu alikua akariri freestyle yeye anachana kuendana na tukio analoliona mbele. Chidi benzi ni mkali haswa japo na uropokaji wake alisema Ngwair sio mtu wa kawaida hapa Tanzania. Chid benz alisema namshinda kukaa chini kuandika mistari, ila kuchana jamaa hana mpinzani, unaweza ukamwacha maskani asubuhi anachana wewe ukaenda dodoma ukarudi jioni ukamkuta anendelea kuchana bila kurudiarudia yoo yo yo yo. Mungu ampunzishe Ngwair.
 
Sahahi mkuu
 
Albert Mangwair alifahamika zaidi kwa jina la Ngwair, alifariki takribani miaka 7 iliyopita huko Afrika Kusini alipokuwa kwa shughuli zake. Alitamba kwa vibao vikali kama ‘She got gwan’ ‘gheto langu’ na ‘Mikasi’

Alikuwa ni mmoja wasanii katika kundi la Chamber Squad akiwa yeye, Dark Master, Mez B (Marehemu pia) na Noorah

Marehemu Ngwair alikuwa amepata umaarufu mkubwa katika ulimwengu wa hiphop kutokana na uwezo wa kufanya mitindo huru, ‘free styles’ na ndipo alijiita cow-weezy, kwa kujifananisha mitambao ‘styles’ na Lil Wyne, aliyekuwa anajiita Lil Weezy

Leo ni kumbukumbu ya kifo chake, Je wewe unamkumbuka Mangwair kwa jambo lipi, Mstari upi wa #Ngwair unaukumbuka, Wimbo upi uliupenda
 
Back
Top Bottom