Albert Mangwea (Special Thread)

Mitungi, mikasi na blanti urithi aliotuachia marehemu.
 
Yule asiye na dhambi kabisa na awe wa kwanza kurusha jiwe.


Tunasubiri aliye mkamilifu aje kutuonya kwenye mambo yetu ya kipuuzi,kijinga na kipumbavu tunayofanya? Watoto wenu mnawaleaje ikiwa hamwezi kuwanyoshea kidole wanapokengeuka!...
Leo mtoto wako akikuuliza umpe sifa za marehemu kwa sababu unaogopa kuhukumu..utamwambia mtoto marehemu alikuwa pastor na alienenda katika njia ipasayo? No wonder we are the rotten society already sababu tunakwepa wajibu wetu ulio wa mhimu na wa lazima kuufanya.
 

Huo wajibu tunasubiri mtu afe ndio tuufanye?
Ninachokipinga mimi ni lugha za matusi kwa marehemu, kwa nini hamkupaaza sauti zetu kipindi yuko hai?
Mlisubiri afe ndio mtukane?, eti alijiona yuko juu, ndio nini hicho?

Mngekuja na mapendekezo ni namuna gani tufanye kuwasaidia ndugu zetu wanaotumia madawa, hapo ningewaelewa.
Sikatai kuusema ukweli wa kilichosababisha kifo cha marehemu ili na wengine wajifunze, lakini sio kwa njia ya matusi na kebehi
Kukaa tu na kungojea mtu afe ndio upate nafasi na kumkejeli na kutukana eti mpumbavu kafa na maneno mengi yasiyopendeza sio ustaarabu hata kidogo.
 
Hii tabia ya kuwa mna msifia mtu anapo kufa tuiache MANGWEA hakuwa mtu mzuri ninaimani watu alio washawishi kuingia kwenyekundi la kutumia madawa ni wengi sana, kama tulikuwa tunampenda kwa kiasi hiki, mbona tulimuacha na hakusaidiwa kama RC?,

hata ww mm cjui mazuri yako hata moja,mazuri ya ngwear wanayajua wanafamilia na watu aliowaiwasaidia kwangu burudani toka kwako ndicho furaha yangu sasa kama unataka kujua mazuri yake hebu tafuta wasanii wenzie na wanafamilia pia,kwa mm heri ya ngwear kuliko wewe
 
Acha kukurupuka soma uelewe nilimaanisha nini.

Mimi sijakurupuka, nimekushangaa unapokomenti vitu vya ajabu ajabu, eti maiti ichapwe viboko, nilitarajia labda utakuja kuomba radhi, maana nilihisi labda umepitiwa tu.
Hujafa hujaumbika ndugu, ni Mungu pekee anayejua wewe utakufa kifo cha aina gani, kukejeli marehemu ni dalili za kutindikiwa.
 
nafikiri hizi kelele zinazopigwa kuhusiana na kifo cha marehemu zingeelekezwa kwa mabosi wanaofanya biashara ya madawa ya kulevya, sababu wao ndiyo source ya vijana kupotea.
 
hakuna hatamu moja anae mtukana Ngwea ukisoma kichwa cha habari utajua, nilicho lenga nikuwa tungemsaidia Ngwea kama RC yawezekana tungekuwanae leo. lakini,kwanini tunamuita shujaa kwalipi kwakubwia unga? mjuni
 
Last edited by a moderator:

Bora umenisaidia mkuu, nashangaa watu wanaotoa lugha mbaya kwa marehemu utamaduni huu wameutoa wapi,
Baada ya kuulizwa amepokeaje kifo cha Osama, Membe alisema hatuna utamaduni wa kufurahia vifo vya watu,
Leo hii hawa ndugu zetu kwa wasababu wao Mungu bado anawajalia pumzi, kufurahia kimya kimya tu wameshindwa wameamua kuingia mtandaoni na kukejeli marehemu, kejeli zinazoashiria chuki binafsi.

Marehemu alikuwa na mchango katika jamii, kuna watu walimpenda, kuna ndugu na jamaa zake bado wanamajonzi makubwa, leo hii wewe unaanza kutoa matusi.

Hata kama alikuwa na madhaifu yake, kila mtu anamadhaifu yake, hakuwa jambazi, lugha mbaya haikubaliki.
 
nafikiri hizi kelele zinazopigwa kuhusiana na kifo cha marehemu zingeelekezwa kwa mabosi wanaofanya biashara ya madawa ya kulevya, sababu wao ndiyo source ya vijana kupotea.

Nahao ndio walio andaa mapokezi yake. mtuwao
 

Umhimu wa mtu unaonekana kutokana na mwitikio wa jamii, sio kama unavyotaka wewe, imekuuma eeeh!
 
Mwana mtoka pabaya!
Yan kwa jinsi unavyoongea tu lazma utakuwa na mwanya wewe!


Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
unamtoa mwenzako kibanzi wakati wewe una boliti kwenye macho yako, jiangalie wewe na nafsi yako je ukifa sasa utaiona pepo au umekalia kumsema mfu ambaye hasikii wala haoni tengeneza njia yako sio kusema marehemu wa watu. Je angekuwa ndugu yako ungefurahia kusikia maneno hayo. Mwenye aliamua kushika njia yake ndio aliona ni sahihi kwake na wewe shika njia yako
RIP mangweha

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Wala msigombane!
Mwenzetu katangulia mbele za haki!
Naamini kwamba kuna mema aliyoyatenda ambayo tunapaswa kujifunza kutoka kwake.
Na yale mabaya tuendelee kumuombea rehema mzigo huu upungue kwake.
Mungu ndiye mwenye maamuzi kwake na kwetu pia.
Tusiiishie kumhukumu kwa mabaya aliyotenda, kila mtu ana mapungufu yake.
 
Hii tabia ya kuwa mna msifia mtu anapo kufa tuiache MANGWEA hakuwa mtu mzuri ninaimani watu alio washawishi kuingia kwenyekundi la kutumia madawa ni wengi sana, kama tulikuwa tunampenda kwa kiasi hiki, mbona tulimuacha na hakusaidiwa kama RC?,

Binafsi nakupongeza kwa kusema ukweli. Ila sidhani kama walioshabikia upuuzi huu ni RC tu. Wabaya zaidi ni viongozi wanaotakiwa kusimamia sheria. Watu wa dini kutegemea imani zao, kumwombea mkosefu si jambo baya. Kinachouma ni viongozi wanaosimamia sheria kushabkia upumbavu huu na kuendeleza dhana ya kupumbaza umma kuhusu dawa za kulevya.

Nilishangaa kumwona bendera Joel akiwa mstari wa mbele kushabkia madawa ya kulevya. Hawa ni viongozi wanaotakiwa kusimamia sheria. Huyu jamaa alitakiwa kuzikwa kama mbwa na hakukuwepo haja ya maandamano na mbwembwe zote.
 
Yote kwa yote teja ngwea limejiua lenyewe kwa misifa yake .mbona sijaona mkipanda fastjet kwenda kumuona teja aliekuwa mahututi au kuna biashara ilikuwa inafanyika kupitia marehemu .Komeni kusifia ujinga

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 

kwanza si kweli kwamba watu hawakuwahi kupiga kelele kuhusu marehemu,jaribu ku search thread utaziona...
Pili,ustaarabu ujue ni jambo gumu kidogo kulifafanua:kwamba mtu anapofariki yale mabaya aliyoyafanya ili kuwa mstaarabu tunayaita Mazuri! Ya kipumbavu yawe ya kielevu au inakuwaje?
Suala mhimu ni kwamba jamii yetu imepotoka pakubwa sana,watu wanaousema na kuuishi ukweli ni wachache sana,sababu ukweli tabia yake kubwa huwa HAUPENDWI...kusema kwamba umhimu wa mtu katika jamii unadhihirishwa na idadi ya watu kwenye msiba ni kweli sababu kwa sasa nchi yetu wala UNGA na watembea UCHI ni wengi mno na hiyo uliyoshuhudia ni asilimia ndogo sana lakini je,uwingi wa wahudhuriaji unabadili msiba kuwa harusi? Laa hasha. Tutamuombea lakini matendo yake na kama alitubu au laa ndiyo yataamua sehemu yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…