Albert Mangwea (Special Thread)

Albert Mangwea (Special Thread)

Kama una akili nzuri huwezi kubisha ufalme wa Ngwea kwenye Hiphop.
Nikikumbuka alivyoichanachana biti ya majani akirap verse ya kwanza kwenye nyimbo MSELA aliyoshirikishwa na TMK Wanaume enzi hizo ni noumaaa!!!
Huwa narudiarudia verse ya Ngwea bila kuchoka.
Ule wimbo ni mzuri sana aisee, kipande cha Albert unaweza kurudia zaidi ya mara 10
 
Wana chamber mnaona muda shaa unayoyoma

Ngwair alikuwa talented levo nyingine kabisa

Katika siku nilizowah kuwaza ujinga ni siku aliyokufa

Niliwaza Kwa nini M2tha P ndo asingeenda ? (bro M2P utanisamehe kama utaona hii comment


Mwaka 2015 M2the P akatumia siku ya kumbukumbu ya Ngwair kuachia kibao chake, nilihairisha kila kitu ili nimsikie, nikaona anaimba umbufi tu nyimbo ya bata bata, Nikajisemea moyon lait kama Israel Mtoa roho angekosea hesabu siku ile then leo (hyo siku) Ngwair ndo awe anahojiwa kwa mara ya kwanza tangu ampoteze mchiz wake na tangu anusurike na mauti, Ukute Kuna Bonge la Ngoma lingetambulishwa leo,

Matokeo yake ni huu uchafu nao usikiliza

Ila kwenye Bwii M2the P ulijitahid kias
Mawazo kama yako na mimi nilikuanayo aisee Mungu atusamehe kuingilia kazi yake japo kimawazo
 
Vizuri. Ila usituaminishe kwamba Ngwair ndiye mwanamuziki wa kwanza kuimba au kurap kwa kubadilisha nyimbo za kingereza. Wakati tunawajua watu kama Swalehe/Sele Jabiri pamoja na makundi mengine ya wakati huo.
Hivi yuko wapi sele, nilikrem nyimbo zake zote zile...opiipii nk hahaha long time
 
baadaye wakakutana dar na kuunda chamber squard.(nimjuavyo noorah ntaelezea siku nyingine).

G-SOLO ambaye yeye ndio alikuwa mwanamuziki mkubwa kipindi hicho Dodoma.siku nikipata muda nitaiongelea East zoo kadri niijuavyo.

mwaka wakitoka wanamuziki wengi ni 5 (ntakuja kuwataja wanamuziki waliofanikiwa mwaka 2003).
 
Huyu mwamba apumzike kwa amani.kwa sisi wa dodoma alituwakilisha vyema mpaka leo najiita mwanachemba mitaa ya eas zu..kuna mstari anasema najivunia nilichonacho kawaidaaa yangu sionekani kwa jicho kwa mtu yoyote mi nakaa mzima,kichaa ata hao mnaowaita mapapaa,mmaza au sista duu anayeng'aa sijali mwembamba au bambataa,mwenye miguu ya vimini,magwiji na wote walio na majina mjini(masupastaa)wenye fedha,viongozi wa dini nikiwapata nasambaa kiulani...wimbo wa bado nipo(ukimwi)na top in dar (TID)...ninaaaa ngwea hatari mno
 
"wengine mnapenda sana vya kupewa ndo maana wengi wenu mnaishia kuchezewa mnamegwa mnaachwa na hata mkiolewa, ndoa inajaa visa na kuonewa na ukinletea kibesi tu asubuhi talaka kwenu, najua huna kitu zaidi ya begi lako (mfuko wa rambo)...."

Albert alikuaga mnoma jo!
unaitwaje huu?
 
Mwanzonimwanzoni nilipata kumsikia kwenye nyimbo za Chamber Squad 1.Boss na 2. Yote Maisha.

Aliangusha flow matata na mistari ya kufufuka mtu.
Hizi nyimbo mbili nazitafuta hadi leo na sujui kwa kuizpata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imetimia miaka 7 leo tangu amefariki Dunia Mwanamuziki nyota wa muziki wa kizazi kipya(Bongofleva) Albert Mangwea.Mangwea alifariki nchini Afrika Kusini alipokwenda kwa shughuli za muziki, Taarifa ya Daktari ilieleza kuwa Bingwa huyo wa Hip Pop na 'Free Style' alifariki kwa sababu ya matumizi ya Dawa za kulevya na Ulevi yaliyopita kiwango( Alcohol and Drug Overdose).

Ghetto langu na Mikasi ni nyimbo zake zilizotamba sana.
 
Back
Top Bottom