Albert Mangwea (Special Thread)

Albert Mangwea (Special Thread)

Kwani rc tulimsaidia wote ama alisaidiwa na kaka mkuu? Huu ujumbe ni wa kaka mkuu. Haendi kwenye misiba ya maprofesa anaenda kumzika kanumba. Kwanza sijui kwa nini hakwenda kumzika ngwear


Alikuwa kwenye "kutembeza bakuli" Japan....
 
Kwangu mimi, kusoma wasifu wa marehemu sio WADHIFA. Na unaongea hivyo kwa kuwa hunijui hata kidogo. Sina kawaida ya kupepesa macho wala kung'ata maneno.

Hii jamii imeharibika na utandawazi kiasi mmeona kwamba, usipoweka wave kwenye nywele na kuvaa suruali chini ya ------ basi wewe hujawa kijana. Mnasifiana ujinga na kuyaacha yaliyo na tunu kwenu.

Huyu kafa kwa ujinga wake na sio kwa kukosa dawa kiasi tumzungumzie kwa hisia za kumuonea huruma. Wote tutakufa kwani kufa ni ada, lkn kufa kipumbavu ni dhalili ya utu wako mwenyewe.

Mmejazana pale uwanjani kila mmoja anasema Mungu amuweke mahali pema peponi, mnasema kwa kumaanisha au kwa mazoea?

Wakati Mandela anasema mwanae amekufa kwa ukimwi ina maana hakuwa mstaarabu? Ustaarabu na unafiki ni mambo mawili tofauti. Nikifa kesho kwa ulevi, walioko nyuma yangu na waambiwe ili wajifunze kuwa unywaji wa pombe sio 'wadhifa' bali ni upuuzi...FULL STOP; NUKTA

Unavyoongea kwa kebehi na majivuno ni kana kwamba mwenzetu umeshajihakikishia kwamba utaingia peponi na tayari ulishamhukumu Marehemu kwamba yeye ni wa motoni. Hata kama marehemu alikuwa anatumia unga, je hakuna watu wasio tumia unga na wana dhambi nyingi na kubwa kuliko marehemu?

Nimesikitishwa sana na posts zako za leo.
 
Unavyoongea kwa kebehi na majivuno ni kana kwamba mwenzetu umeshajihakikishia kwamba utaingia peponi na tayari ulishamhukumu Marehemu kwamba yeye ni wa motoni. Hata kama marehemu alikuwa anatumia unga, je hakuna watu wasio tumia unga na wana dhambi nyingi na kubwa kuliko marehemu?

Nimesikitishwa sana na posts zako za leo.
Mjuni Lwambo hivi wafikiri kunatakiwa tubembelezane kwenye kuonyana?? binafsi huwa naamini kuonya kwahitaji ukali na ni heri kuonyana kuliko kupongezana. Mwana Mtoka Pabaya hajasema kwamba yy ataenda peponi lkn ameonya hakuna haja ya sisi kubembelezana hata kwenye makosa yetu. ingekuwa huyu Ngwea alijirekebisha na kuwa kijana bora basi leo hii tungemsifia sana lkn pamoja na maangazo na mafundisho yote still alikaid je wataka leo hii yasisemwe wazi kwaajili ya kuwasaidia wengine??
 
Last edited by a moderator:
Mtu akikupiga ngwala akakuangusha kwa lengo la kukuchelewesha mashindanoni, hilo ni kosa lake, lakini wewe uliyeangushwa kuendelea kukaa hapo chini ni UPUMBAVU wako.

Hakuna aliyesema kwamba yeye ni mtakatifu, lakini kuna mambo yapo wazi na si ya kuyaunga mkono. Ngwea hakutumia madawa sababu ya kukosa kwake elimu juu ya madawa bali alitumia madawa kwa fahari ya maisha yake. Watu kuleta madawa ya kulevya si kisingizio cha wewe kuyatumia na kujiita muhanga.

Ashakhum si matusi 'wengine wameleta condom, haya kanunue basi ujamiiane na ndugu zako kwa kuwa si kosa lako ni kosa la walioleta condom sokoni'

Vijana tutumie vyema akili zetu. Yule mpumbavu aliyekufa, ana wapumbavu wengine wengi nyuma yake. Ili wapumbavu mliobaki muelewe dhahama ya upumbavu, ilipaswa sababu ya kifo chake ielezwe pale kwenye kusanyiko na sio kujilizaliza eti Mungu amuweke mahali pema peponi.

Hakuna mtakatifu, lkn jitahidi kusafisha njia zako kadiri uwezavyo. Unafiki ndio unatuponza. Usipende kuelezwa maneno matamu, penda kuelezwa ukweli. Wakati anatumia hayo madawa na kuweka ------ nje wote tuliona ni sawa, ila leo kafa ukweli huo huo haukubaliki.

UNAFIKI NDUGU ZANGU, unafiki mbaya. Issue si ulikufaje, issue ni uliishije. Maisha ya kipumbavu ndio huelezea kifo cha mtu

Labda ninaweza kuhisi kitu,

Kuna wauaji, magaidi na waovu wa kutisha washawahi kupoteza maisha, lakini watu hawakutukana wala kuonyesha jaziba na hasira kali kwa marehemu aliyekwisha kuaga dunia.

Inawezekana ulikuwa na chuki binafsi na Marehemu, sasa naomba nikushauri;
Kumtukana tu hakuwezi kumaliza hasira zako, maana umesema alijiona yuko juu sijui na nini na nini,
Chukua mapanga na mishale nenda kakatekate kaburi lake, kutukana tu mtandaoni haisaidii.
 
Wananchi wa nchi hii wanachekesha sana!!! Wale ma-injinia wanaokufa kazini wakijenga maghorofa hawavumi kama kifo cha msanii tena cha kujiua mwenyewe na maulevi yake. Where are we Tanzanians????
 
Mjuni Lwambo hivi wafikiri kunatakiwa tubembelezane kwenye kuonyana?? binafsi huwa naamini kuonya kwahitaji ukali na ni heri kuonyana kuliko kupongezana. Mwana Mtoka Pabaya hajasema kwamba yy ataenda peponi lkn ameonya hakuna haja ya sisi kubembelezana hata kwenye makosa yetu. ingekuwa huyu Ngwea alijirekebisha na kuwa kijana bora basi leo hii tungemsifia sana lkn pamoja na maangazo na mafundisho yote still alikaid je wataka leo hii yasisemwe wazi kwaajili ya kuwasaidia wengine??
Mkuu, huwezi kumuonya marehemu, wote tu wadhambi, mwenzetu akitutoka tumwombee kwa Muumba asamehewe madhambi yake

Nakuomba pitia tena posts za jamaa, anaandika kwa jazba, ukali na la kusikitisha zaidi anamtukana matusi marehemu, huu sio ustaarabu hata kidogo, kwani yeye ni mwema mno kiasi cha kutukana hivyo?, nimeshawishika alikuwa na chuki binafsi na marehemu, kuna post yake moja amesema marehemu alijiona yuko juu, uthibitisho wa chuki binafsi.
 
Mwana Mtoka Pabaya, unajua marehemu aliendekeza starehe mjini akawa amemtelekeza mwanae dodoma? Uliona mtoto alivyokuwa pale mssibani yani hata mavazi na muonekano alionesha ni mtoto aliyekuwa anaishi maisha ya chini. Wakati huo baba anatanua mjini kwa pombe, mikasi na cock tail (unga........kwenye kampani ya marehemu walikuwa wanaita unga cock tail). Hata kumtambulisha kwa mama yake mzazi alishindwa? katika maisha alishapata akaamua kuzimalizia kwenye kampani na mademu....kweli anastahili sifa huyu? tujifunze kupitia maakosa ya wenzetu ili sisi tusije rudia.

Kuhusu maisha yake ya kiroho ni kweli kwa nje tu hayakuwa ya kuigwa ila hatujui dakika yake ya mwisho aliongea nini na Mungu wake, neema ya kristo ni ya ajabu dakika unayodhani haiwezekani kwa Mungu inawezekana. Kama mwizi aliponea msabani sembuse wengineo.

All in all tunajifunza katika kila kitu, iwe kifo au uzima.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: mzm
mnao msifia Ngwair wote ni wafiki tuu!!Nngwair na yule r,rafik yake M2THEP ni mateja!!!!sasa wanacfiwa kwa lip? kama ciunafikihuo?
 
Luke 6:37, don't judge and you will not be judged, only god can judge him.
 
Kweli umepolomoka tena kivyote kiakiri hatari kiafya mana naamini utakua na mtindio wa ubongo ambao unasababisha kusema mambo bila kufikiri
 
kwa maoni yangu mi nilitaka maiti yake ichapwe viboko ili liwefundisho kwa mateja ote na wanao taka kuingia ktk mkumbo huo, binafsi hakuna jema nililo jifunza kwake kamakweli alikufa kwa madawa.
Acha kiburi, hivi mama Yako Akifa kwa ukimwi utaichapa bakora maiti yake kwa kua ni muasherati?
 
Wananchi wa nchi hii wanachekesha sana!!! Wale ma-injinia wanaokufa kazini wakijenga maghorofa hawavumi kama kifo cha msanii tena cha kujiua mwenyewe na maulevi yake. Where are we Tanzanians????
ndugu umenena vema -kwa ufupi hatuhitaji na hatuna muda na wenye juhudi na maarifa- hakika safar yetu ndefu
 
Who told you kuwa ukifa dhambini unakwenda kupumzika?!!Mshara wa dhambi ni mauti tena ya milele motoni,
msijidanganye na lugha yenu ya kipuuzi ya R.I.P,hakuna mtu anakwenda kupumzika kama anafia dhambini,
mnataka kwenda sehemu nzuri baada ya kufa Mungu anasema muache dhambi mumpokee Yesu ili muende
hiyo sehemu nzuri hakuna namna nyingine ya kupumzika hata mngezikwa na dunia nzima

actually, anapumzika! Siku ama kipindi cha ku-pay for our sins bado... For now everybody who dies Rest in Peace! and no one wil ever going to heaven by the way!
 
Nimesikitishwa sana na huu uzi pamoja na baadhi ya comments za wadau. Kuna watu humu wanajifanya wao ni watakatifu kiasi cha kunyooshea vidole wengine na pia kumlaumu marehemu. Ngwair ni mmoja wa mamilioni ya watz wahanga wa hayo madawa. Kwanini tulaumu wanywaji wa vilevi huku tukisifia viwanda vinavyotengeneza hivyo vilevi?

Mapokezi na mazishi waliyomfanyia ni kama shujaa kitu ambacho SI KWELI. Utafikiri amekufa akiwa vitani anatetea tanzania!!! Huu ni upuuzi! Nyimbo zake (na wasanii wengine wa bongo flavor) hazina tija wala umuhimu kwa wadogo zetu. Zaidi nyimbo zinachochea uzinifu, ulevi wa pombe, kuvaa heleni kama mashoga, suluali kata K, na uchafu woote wa ku angamiza jamii na utamaduni wetu. Huu mtindo wa wasanii uch.wara kujifanya ma supa staa na kupelekana Viwanja vya Leaders pindi wanapokufa itabidi ukome. Kuna watu muhimu sana katika maendeleo ya taifa hili wanaostahili kupewa heshima zaidi pindi wanapokufa, sio hawa wasa.nii
 
Luke 6:37, don't judge and you will not be judged, only god can judge him.

Biblia ni moja lakini inasomwa na watu tofauti,wenye uelewa tofauti hivo uwezekano wa tafasiri tofauti...
Tunasubiri aliye mkamilifu aje kutuonya kwenye mambo yetu ya kipuuzi,kijinga na kipumbavu tunayofanya? Watoto wenu mnawaleaje ikiwa hamwezi kuwanyoshea kidole wanapokengeuka!...
Leo mtoto wako akikuuliza umpe sifa za marehemu kwa sababu unaogopa kuhukumu..utamwambia mtoto marehemu alikuwa pastor na alienenda katika njia ipasayo? No wonder we are a rotten society sababu tunakwepa wajibu wetu ulio wa mhimu na wa lazima kuufanya.
 
kwa maoni yangu mi nilitaka maiti yake ichapw viboko ili liwefundisho kwa mateja ote na wanao taka kuingia ktk mkumbo huo, binafsi hakuna jema nililo jifunza kwake kamakweli alikufa kwa madawa.

Alikuwa Japan na Singapore ndo maana hakuweza kuhudhuria ila amekosa picha na "masupasta" wa bongo movies na music
 
Back
Top Bottom