Nairobi – Kesi ya mauaji ya Albert Omondi Ojwang imeanza kusikilizwa katika Mahakama Kuu ya Kibera, huku ushahidi wa kwanza ukitoa picha mpya kuhusu kile kilichotokea ndani ya Central Police Station.
CCTV technician Aloni Okwako aliiambia mahakama kuwa alipofika kituoni mnamo Juni 9, 2025, alikuta DVR (Digital Video Recorder) ya CCTV ikiwa imezimwa baada ya power cable kutolewa.
Baada ya kuirejesha kuwaka kwa maelekezo ya maafisa wa IPOA, alijaribu kuretrieve footage ya Juni 6 na 7 lakini hakupata recordings zozote.
Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, DVR ilikuwa imeformatiwa, meaning footage yote ilikuwa imefutwa.
Pia alibaini baadhi ya internal components za kifaa zilikuwa zimeondolewa kabla ya uchunguzi kukamilika, jambo ambalo linaibua maswali kuhusu uwezekano wa kufichwa kwa ushahidi.
Wakati huo huo, Director of Public Prosecutions (DPP) aliambia mahakama kuwa upande wa mashtaka utathibitisha kuwa Albert Ojwang aliletwa Central Police Station akiwa hai, lakini baadaye alipigwa na kuuawa akiwa ndani ya cells.
DPP anadai kuwa baada ya kifo hicho, kulikuwa na jaribio la kuficha kilichotokea, ikiwemo kufutwa kwa CCTV footage.
Albert Ojwang, aliyekuwa mwalimu na mwanablogu, alikamatwa kufuatia uchunguzi kuhusu chapisho la mtandaoni.
Alifariki akiwa chini ya ulinzi wa polisi katika mazingira yaliyozua hasira nchini, maandamano ya wananchi, na wito wa haki kutoka kwa makundi ya kutetea haki za binadamu.
Uchunguzi wa baadaye ulionyesha kuwa majeraha aliyokuwa nayo hayakuendana na madai ya awali kwamba alijijeruhi mwenyewe akiwa ndani ya police cell.
Kesi hiyo inaendelea huku Wakenya wengi wakifuatilia kwa karibu wakisubiri ukweli kuhusu kilichosababisha kifo cha Albert Ojwang na iwapo waliohusika watawajibishwa.
Source: Tuko.co.ke