Wakati wa mchakato wa kutia nia kwa wana CCM kuomba kugombea ubunge kwa majimbo mbalimbali ya Tanzania, mwana-CCM Alex Msama Mwita alikuwepo akilitaka Jimbo la Ukonga ambalo lipo jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, Msama aliachwa kwenye majina yalirudi jimboni kwa ajili ya kura za maoni ambapo mbunge aliyemaliza muda wake, Jelly Silaa aliongoza na sasa ndiye mgombea wa jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi.
Katika hali ya kuonesha mshikamano na siyo uadui, Msama alitoa kauli akikubali matokeo na kuwataka watia nia wenzake walioachwa kushikamana na kumuunga mkono yule atakayepita kwenye kura za maoni.
Kama hiyo haitoshi, Msama alisema yeye ni mwana CCM kindakindaki, hawezi kukihama chama hicho ambacho yupo miaka na miaka. Sasa katika hali ya kushtusha, Septemba 2, 2025 kuna taarifa zikasambaa mitandaoni zikidaiwa kutolewa na Chama cha Chaumma zikiweka wazi majina ya wanachama wake ambao watagombea ubunge nchi nzima wakishindana na wagombea wa CCM.
Katika orodha hiyo, jina la Alex Msama Mwita lipo. Kwamba ni mgombea katika Jimbo la Ukonga ambalo yeye alitia nia kupitia CCM. Hii ina maanisha kuwa, Msama amehamia Chaumma kutoka CCM.
Majina hayo yalianza kwa kuandikwa; ORODHA YA WAGOMBEA UBUNGE WA CHAUMMA HII HAPA.
Yalianza majina ya wagombea ubunge wa Mkoa wa Pwani na majimbo yake yote 7.
Ukafuata Mkoa wa Dar es Salaam na majimbo yake yote 12 kama ifuatavyo;

DAR ES SALAAM:
8: BENSON KIGAILA (KIVULE).
9: HERMAN KILOLOMA (CHAMAZI).
10: YERICKO NYERERE (KIGAMBONI).
11: Khadija Nyamwago (MBAGALA).
12: Agnester Lambeth Laizer (SEGEREA).
13: Dorcas Francis Mlavu (KAWE).
14: EDWARD KINABO (KIBAMBA).
15: Moza Ally (KINONDONI).
16: SAMWEL PETER BUKURA (TEMEKE).
17: ALOYCE KIBONA (UBUNGO).
18: Shadya Masoud Mkola (ILALA)
19: ALEX MSAMA MWITA (UKONGA).
Orodha hiyo imezua mshangao kufuatia mhusika mwenyewe, Alex Msama Mwita kukanusha vikali kwamba siyo kweli. Ni uongo.
"Hiyo orodha siyo ya kweli ni ya uongo kwenye eneo la jina langu. Mimi sigombei Ubunge kwa Chaumma wala siyo mwanachama wa Chaumma," alisema Msama.
Akaendelea: "Ingekuwa kweli ningeita waandishi wa habari kuwaeleza kwamba nimeamua kuhamia Chaumma na kugombea ubunge. Mimi bado ni mwana CCM imara kabisa. Tena natoa wito kwa Watanzania wote tujitokeze kwa wingi Oktoba 29 mwaka huu kumpigia kura za Ndiyo mgombea wetu wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan ili amalizie pale alipoanza," alisema Msama.