ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
Mwaka 1833 nchini Sweden alizaliwa mtoto aliyeitwa Alfred Nobel. Huyu jamaa baadaye alikuja kuwa mwanakemia, mhandisi, mvumbuzi na mfanyabiashara mkubwa. Chanzo kikubwa cha utajiri wake kilikuwa teknolojia ya vilipuzi, hasa baada ya kuvumbua dynamite mwaka 1867. Teknolojia hii ilitumika kwenye uchimbaji wa madini, ujenzi wa reli, barabara na miradi mikubwa ya miundombinu. Nobel alikuwa na hati nyingi za uvumbuzi (patents), viwanda na biashara katika nchi mbalimbali.
Sasa sikiliza hapa! Alfred Nobel hakuwahi kuoa wala kupata watoto. Alipofariki mwaka 1896, aliacha utajiri mkubwa sana. Katika wosia wake, aliagiza sehemu kubwa ya mali yake, takribani milioni 31 za kronor za Sweden, iwekezwe na mapato yake yatumike kila mwaka kuwazawadia watu waliotoa mchango mkubwa kwa manufaa ya binadamu.
Mwaka 1900 ikaanzishwa taasisi inayoitwa Nobel Foundation, ambayo kazi yake ni kusimamia utajiri huo na kuhakikisha tuzo zinaendelea kutolewa. Mwaka 1901, tuzo za kwanza za Nobel zikatolewa katika Physics, Chemistry, Medicine, Literature na Peace. Tuzo ya Economics iliongezwa baadaye mwaka 1968 kwa ufadhili wa Benki Kuu ya Sweden.
Cha kunishangaza zaidi ni kwamba miaka zaidi ya 120 imepita tangu tuzo za kwanza zitolewe, lakini mfumo huu bado unaendelea! Fedha alizoacha Nobel hazikuwa zinaondolewa tu kila mwaka mpaka ziishe. Ziliwekezwa, na kupitia usimamizi wa uwekezaji huo, taasisi imeendelea kuwa na uwezo wa kugharamia zawadi na shughuli zake.
Leo hii, mshindi wa Nobel anaweza kupata mamilioni ya fedha, medali na heshima kubwa duniani. Na kumbuka, mtu aliyekuwa chanzo cha utajiri huo alifariki zaidi ya karne moja iliyopita!