Alfu Lela Ulela, Shakespeare na Irving Wallace Ndani ya "Posa za Maana"

Alfu Lela Ulela, Shakespeare na Irving Wallace Ndani ya "Posa za Maana"

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
ALFU LELA ULELA, WILLIAM SHAKESPEARE NA IRVING WALLACE WANAPOJUMIKA PAMOJA KATIKA KITABU CHA TUNE SHAABAN SALIM ‘’POSA ZA MAANA’’

Juzi niliandika na kusema kuwa kitabu hiki kina mwendo mkali.

Kila ukifungua ukurasa mmoja ukurasa wa pili unakuita kwani akili yako inakuwa imetekwa unataka kujua ukurasa wa mbele una nini?

Nilipoanza kukisimulia kitabu hiki nilisema kuwa namuona William Shakespeare ndani ya kurasa zake.

Jana nimekutana na maajabu mengine.

Nimewasoma waandishi wa Alfu Lela Ulela na Irving Wallace ndani ya kitabu hiki.

Najiuliza haya yanawezekanaje?

Kalamu ya Tune inazungumza maneno ukayasikia hasa masikioni kwako si kama kalamu yake inaandika herufi peke yake.

Bwana Khamisi kapwelewa na suala la posa ya binti yake mdogo.

Anatakiwa achague elimu ya bint au ndoa ingawa Bi. Salma yeye keshalitolea uamuzi kuwa bint anakwenda kwa mume mwenye fedha tena anaishi Ulaya.

Turejee kwa Bwana Khamisi na mkewe Bi. Salma.

Bwana Khamisi kapwelewa lakini anatolewa dunia hii ya mji wa Tulieni anabisha hodi na kuingia mji wa kusadikika, mji wa Ali Nacha.

Bwana Khamisi hayuko tena Tulieni.

Anaota enzi zake ana kazi ya maana kazi aliyoipoteza kwa kufukuzwa.

Kisa cha kufukuzwa kazi ni shutuma kuwa yeye ni mfuasi wa chama cha upinzani.

Hapa sasa Tune anamwingiza msomaji katika staili nyingine kabisa ya uandishi, staili ya Irving Wallace.

Irving Wallace kama Tune ni mwandishi nguli wa riwaya.

Irving Wallace anaandika kweli kama riwaya kutokana kweli ndani ya jamii.

Vitabu vyake vikawa maarufu ulimwengu mzima na vikatengenezwa filamu.

Staili hii yake ya uandishi Irving Wallace akawa anawananga watu wazito katika jamii akiwa kajificha kwenye kupiga hadithi na hivyo anabaki salama hana wa kumlaumu.

Tabu mtu kupeleka kesi mahakamani kwa madai kuwa hadithi ile ya Esopo imemlenga yeye.

Mwandishi anaeleza nema zilizokuwapo Tulieni zamani na dhiki zilizokuja baadae.

Lakini mwandishi anamwachia msomaji atumie akili yake kutegua kitendawili alichokitega anapoeleza nema zilizokuwako Tulieni.

Mwandishi halikadhalika anaeleza dhiki zilizokuja za njaa na ufukara na mwishowe dhiki iliyotamalaki ya watu kufukuzwa kazini kwa hisia kuwa haungi mkono serikali iliyoko madarakani.

Bwana Khamisi akiwa ndani ya ndoto anakumbuka ofisi yake iliyokuwa na kiyoyozi.

Bwana Khamisi anakumba akiwa ndotoni afueni ya maisha yake na anajiangalia hali yake ya sasa.

Ali Nacha katika ndoto.

Ali Nacha akiwa sokoni kasinzia jua kali linampiga akisubiri wateja waje kununua bidhaa zake za vikombe na sahani za udongo akawa anajipa matumaini kuwa biashara yake ile itamtajirisha na atakapokuwa tajiri ataona mke mzuri.

Halikadhalika Bwana Khamisi juu ya dhiki ile ya kutawaliwa na serikali isiyojali haki za raia wake ndoto inampeleka katika fikra kuwa safari hii chama chake kitashinda uchaguzi.

Chama chake kikishinda uchaguzi kitakuwa madarakani na yeye atarejeshwa kazini, maisha yake yataboreka na ataoa mke mwingine au wake kukomesha kidomodomo na ndambi za Bi. Salma anaemweka roho juu.

Kitabu huwa kinakuwa na ladha kinapoeleza ukweli wa maisha ndani ya jamii.

Kitabu hiki kila herufi, kila sentensi, kila mstari umebeba elimu na historia ya yale yawakutayo watu katika maisha yao ya kila siku.

Tune analieleza darasa lililojaa wanafunzi na anasema samani iliyoko kwenye darasa lile ni meza na kiti cha mwalimu.

Meza na kiti cha mwalimu.
Mwandishi anakusudia nini?

Darasa halina madawati wanafunzi wamekaa chini?

Mbona hakuandika hivyo?

Kalamu imepata mwandishi.
Hakika ashiki kitabu hiki.

Hadithi njoo utamu kolea.
 
Back
Top Bottom