Algeria kuwakosa nyota wake wa Porto na Valencia

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Wapinzani wa Taifa Stars kwenye mechi ya mchujo wa kuwania kufuzu kombe la Dunia, timu ya Algeria imepata pigo la kuwakosa nyota wake watatu wanaocheza vilabu vya Porto, Valencia na Dynamo Zaghreb.


Nyota wa Porto, Yacine Brahimi akipambana na Sami Khedira

Kwa mujibu wa tovuti ya shirikisho la Algeria, wachezaji tegemeo, Yaccini Brahimi ( Porto), Sofiane Felghouli (Valencia) na El Soudani hawataweza kucheza pambano la Jumamosi dhidi ya Taifa Stars.

Wote watatu ni majeruhi hivyo kukosa pambano hilo la mtoano litakalochezeshwa na mwamuzi kutoka Mali.

Msafara wa Algeria unatarajiwa kuwasili nchini siku ya Alhamis kwa ndege binafsi ya kukodi, ukiwa na jumla ya watu 65 wakiwamo wachezaji 24.

Chanzo: Soka360
 
basi hapo wachezaji wetu ndo wataingia uwanjani kana kwamba wameshinda kwa goli 10-0.
 
Ni kweli mkuu? "isije kuwa propaganda za mechi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…