Alhad Salum alia na Mwamposa kuwaombea wanawake wa kiislamu, awataka mashehe waanzishe vilinge vya dua kuwaponya wanawake!

Alhad Salum alia na Mwamposa kuwaombea wanawake wa kiislamu, awataka mashehe waanzishe vilinge vya dua kuwaponya wanawake!

Mimi Sina tatizo na uislamu ila waislamu wengi wana unafiki Sana naishi nao muda mwingi sana..

Kuna mtu mmoja akanijibu eti pale kwa mwamposa hakuna muislamu anayeenda hata mmoja wale ni mamluki tu Wala siyo waislamu.Muislamu halali hathubutu kukanyaga kanisani maana ni haram,nikaamua kumpotezea badala ya kubishana

Huyu shehe ndy ameona mbali na ameukubali ukweli kwamba Kuna wamama wengi Sana wa kiislamu wanaenda kwa mwamposa so tyr Kuna tatzo na wao Kama viongozi wa kiislamu na waislamu wote wanapaswa kulitatua..Hizi Mambo za kila linapotokea Jambo wasilolipenda wanasingizia hao siyo' waislamu halitawasaidia hata kidogo'

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Si walisema hakuna nabii kutoka mbeya...naona dawa imeanza kuwaingia..bado wao tu kwenda kukanyaga mafuta mapepo na majini yawatoke.

Hofu yangu wasijiripue tu mana injili haijawahi shindwa na mapepo na majini.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kinachonishangaza kuhusu huyu Bw. Mwamposa huwa hajibu, hajitetei, hafanunui wala hagombani mtu.
Anajua wito wake ndio maana hahangiiki

Kuna wengine hawajui wito wao ndio maana .Yesu aliwatuma wakamhubiri Yesu wao kusimama madhabahuni kuhubiri Mwamposya!!!! Utafikiri Mungu aliwatuma kuwa nendeni mkamhubiri Mwampsya!!

Huyo Mwamposya ndio kiongozi wangu nasali kwake mimi

Ukiona watu wanajaa vile pana kitu wanapokea .Wasomi wamejaa pale wenye hela zao na mali zao Hakuna kanisa inajaa watu wenye magari mengi ya uhakika kama kwa Mwamposya kuonyesha wazi wao sio wajinga

Vilinge vya mashehe vipo Kibao lakini huko hawapati ufumbuzi ndio maana huenda kwa Mwamposya.Kungekuwa na ufumbuzi huko wasingeenda

Hata kwa baadhi ya Wakristo kuna shida mtu anakuwa na Tatizo lake kwenye dini yake alipo hapati ufumbuzi akienda kwa Mwamposya anapata ufumbuzi sio tu anawaambia wengine lakini wanaomjua mtaani kwake wanaona kweli mwenzetu shida yake imeisha.Ndio maana unakuta makundi makubwa anainuka kwenda hayajali cha dini yao wala nini

Tatizo huwa na nguvu kuliko dini lisipopata ufumbuzi

Mwamposya ana ufumbuzi wa matatizo kitiu ambacho baadhi ya viongozi wa dini hawana wanachujua wao kutwa ni kugeuza misikiti au makanisa madarasa tu ya kufundisha Biblia au Kurani na kukusanya sadaka
 
Back
Top Bottom