Kura haziibiwi kwenye kituo cha kupiga kura, kura za Rais zinaibiwa kwenye majumuisho ya nchi nzima.
Hakuna namna yoyote ya kuiba kura mkiwa na mawakala wakweli na mkawa na senta yenu kila kata ya kujumlisha kura za diwani, kura za jimbo na kura za Rais.
Huitaji Tume ya uchaguzi kukutangazia mshindi, mshindi mnamjuws nyinyi wenyewe mkiwa na timu nzuri ya kuratibu ukusanyaji wa nakala za matokeo kila kata, jimbo na mkoa kwa ujumla.
Maalim Seif huwa anakuwa ameshaliza majumuisho ya kura kabla ya Zec na ndio maana Jecha akaona isiwe tabu bora afute uchaguzi.
Nina wasiwasi mkubwa na Chadema sidhani kama wana timu ya uhakiks ya kusimamia kura za urais.
Makao makuu ya Chadema pamepwaya hakuna briefings zozote za uchaguzi badala yake sasa Lisu ndio anaibeba Chadema.
Kwenye uchaguzi uliopita Ukawa walikuwa na ngome yao Kawe kwa ajili ya briefings, kule Kenya Odinga alikuwa na ngome yao waliita Pentagon ndio ilikuwa inaratibu, lakini Chadema sijui tatizo ni nini?
Bila Lisu kurudi ni kweli Chadema ilikuwa inakwenda kupata aibu ya mwaka, ila Mungu mkubwa Lisu amerudi amebadili upepo ccm inakwenda kuangushwa, lakini kuna mikakati gani ya kichama badala ya kumtegemea Lisu kwa kila kitu?