Alhamulilah mada za ujenzi zimeanza kutamalaki jukwaani

Alhamulilah mada za ujenzi zimeanza kutamalaki jukwaani

Ijumaa Kareem! Niwasalimu katika mchakato wa katiba mpya! Katiba ya wananchi sio ya chama chakavu..!!!

Mwenyezi Mungu ametufanyia wepesi! InshaAllah..![emoji1545]hatuna cha kumlipa..! Kuna mabadiliko makubwa, biashara zinafunguliwa! Site zilizododa zinafufuka! Mada za ujenzi zinarejea jukwaani hasa kwenye jukwaa la ujenzi hapa JF na mitandaoni...Mungu ni mwema wakati wote
. Sasa wananchi wanaanza kuulizia ramani za ujenzi
. Sasa wananchi wanaanza kuulizia bei ya viwanja
. Sasa wananchi waanza kuulizia bei za malighafi, gharama za mafundi nk..!
. Sasa Wananchi wanaanza kutangaza kwa nguvu huduma zao kwenye sekta ya ujenzi..!

Yangu ni haya!
Hii hali tunayopitia ni sawa na mahututi kuanza kupata nafuu...!!! Sasa katika hatua hii washauri wabaya na wapigaji hawakosekani.. Naomba ridhaa ya kutoa mchango wangu na ushauri.. Una haki kamili ya kuuchukua ama kuupuuza!
Nakuja na full package! Naomba subra yako.
Swafiii tupe nasaha zako mkuu
 
Swafiii tupe nasaha zako mkuu
Natambua walau sasa wanazengo wanaanza kuwa na chochote kitu mifukoni, baada ya kutoa zile za matumizi ya lazima, matumizi muhimu na zile za matumizi ya hasara...!
Kwa wale ambao hawakuwa na site za kuendeleza wala viwanja ambavyo hawajavigusa kwenye ujenzi ni heri kufanya hivi
Sasa hivi kabla mambo hayabadilika sana, watu wanauza sana nyumba zisizokamilika... Ni vema kununua nyumba za namna hii na kufanya umaliziaji taratibu kuliko kuanza ujenzi mpya.. Hasa kama bajeti inabana
Ujenzi una changamoto nyingi sana, 20M kwenye ujenzi wa nyumba ya kawaida kabisa inaweza isikufikishe popote!
Kuna changamoto ya muda
Kuna changamoto ya usimamizi
Kuna changamoto ya mafundi nknk
Nitaendelea.....
 
Kama ukishindwa kupata site ya kumalizia ama la unataka ujenge nyumba ya ladha yako basi nakushauri fanya haya...
. Fanya manunuzi kwenye maduka ya jumla tuu.. Hapa utaokoa pesa nyingi
. Hakikisha unapata muda wa kusimamia ujenzi mwenyewe
. Kama ni lazima kuwa na msimamizi basi si vema kumuamini asilimia 100.. Na hakikisha humuambii au hajui muda wako wa kwenda site na muda utakaokaa..
. Kipindi cha ujenzi epuka kuwapeleka marafiki na hata ndugu ama kutangaza mitandaoni na sehemu za starehe kuwa sasa uko kwenye ujenzi.. Hakuna uchawi mbaya kama macho na midomo ya watu
. Kipindi chote cha ujenzi badili ratiba ya mavazi, starehe, chakula nk
 
Back
Top Bottom