Alhamulilah mada za ujenzi zimeanza kutamalaki jukwaani

Naona mzee alikubana mirija yenu ya easy money mkanyoka! Anyway chukueni tahadhali ipo siku tutapata chuma kingine
Duuh! zamu yako itafika...
Ukitaka kujua habari za Tajiri, Muulize Masikini
 
Swafiii tupe nasaha zako mkuu
 
Swafiii tupe nasaha zako mkuu
Natambua walau sasa wanazengo wanaanza kuwa na chochote kitu mifukoni, baada ya kutoa zile za matumizi ya lazima, matumizi muhimu na zile za matumizi ya hasara...!
Kwa wale ambao hawakuwa na site za kuendeleza wala viwanja ambavyo hawajavigusa kwenye ujenzi ni heri kufanya hivi
Sasa hivi kabla mambo hayabadilika sana, watu wanauza sana nyumba zisizokamilika... Ni vema kununua nyumba za namna hii na kufanya umaliziaji taratibu kuliko kuanza ujenzi mpya.. Hasa kama bajeti inabana
Ujenzi una changamoto nyingi sana, 20M kwenye ujenzi wa nyumba ya kawaida kabisa inaweza isikufikishe popote!
Kuna changamoto ya muda
Kuna changamoto ya usimamizi
Kuna changamoto ya mafundi nknk
Nitaendelea.....
 
Kama ukishindwa kupata site ya kumalizia ama la unataka ujenge nyumba ya ladha yako basi nakushauri fanya haya...
. Fanya manunuzi kwenye maduka ya jumla tuu.. Hapa utaokoa pesa nyingi
. Hakikisha unapata muda wa kusimamia ujenzi mwenyewe
. Kama ni lazima kuwa na msimamizi basi si vema kumuamini asilimia 100.. Na hakikisha humuambii au hajui muda wako wa kwenda site na muda utakaokaa..
. Kipindi cha ujenzi epuka kuwapeleka marafiki na hata ndugu ama kutangaza mitandaoni na sehemu za starehe kuwa sasa uko kwenye ujenzi.. Hakuna uchawi mbaya kama macho na midomo ya watu
. Kipindi chote cha ujenzi badili ratiba ya mavazi, starehe, chakula nk
 
Kiwanja kimoja kinauzwa maratatu ama kweli Jr nimekuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…