Katibu wa Siasa na Uenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Bananga amesema chama hicho kupitia jumuiya yake ya vijana (UVCCM) wamejipanga kujibu mapigo dhidi ya mtu yeyote wakiwemo makada wa vyama vya upinzani watakaotumia vibaya uhuru wa kufanya siasa kumtukana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine.
Bananga ameyasema hayo akihutubia mkutano wa hadhara Mwananyamala Kisiwani Kata ya Makumbusho jijini Dar es Salaam baada ya kupokea taarifa ya chama kimojawapo cha siasa (hakijatajwa jina) kuvunja jiwe la msingi la moja ya shina ya CCM ndani ya kata hiyo iliyoandaliwa kuzinduliwa na UVCCM Wilaya ya Kinondoni kupitia kampeni yao ya Kijana na Kijani.
Bananga ameongeza kuwa CCM kupitia UVCCM kitawalinda viongozi, wanachama wa CCM pamoja na mali za chama hicho kwa gharama za damu huku akisisitiza kuwa wako tayari kujibu mapigo ya kile alichokiita chokochoko za vyama vya upinzani kwa βstailiβ ile ile watakayokuja nayo.

Kati ya ccm na hivyo vya upinzani nani anaongoza kufanya siasa za kihuni? Kuna ofisi ngapi za vyama vya upinzani hasa chadema bila hatua zozote kuchukuliwa?
Embu acheni ujinga wenu