Ali Choki na Super Nyamwela warudi Twanga Pepeta

Duuu...siamini kwa maneno jeuri aliyokuwa anatoaga Ali Choking kuhusu Twanga wakati yuko na Extra bongo yake sikutegemea leo kama angeweza kula matapishi yake ..yani kaufyata..nn kimemsibu??? kweli ngoma ikiwamba sana mwisho wake hupasuka
 
Huyu si alimtangaza Asha Baraka kuwa mwanamke mwenye roho mbaya kuliko wanawake wote duniani, na kwamba hataenda kwenye maazishi yake, wala Asha hasije kwenye maazishi yake! Imekuwaje tena?
 
Sisi wapenzi tunafurahia Burudani tu, Twanga ni Kisima cha burudani karibu Ally Choki, usiwe unaacha mbachao kwenye msala upitao
 
Kama siasa Wa chadema ataenda Act, Wa Act ataenda CCM, wa CCM ataenda CHADEMA.

KIKUBWA HAPA NI NJAA TU.
 
Huyu si alimtangaza Asha Baraka kuwa mwanamke mwenye roho mbaya kuliko wanawake wote duniani, na kwamba hataenda kwenye maazishi yake, wala Asha hasije kwenye maazishi yake! Imekuwaje tena?

Adui yako muombee Njaa Huyu ndg inasemekena Alikuwa anapata ufadhili tangu Bendi inaanza na jamaa ambaye kwasasa ni Marehem so tangu hapo hajatulia na viingilio vya milangoni sio ishu sana....so kurudi Twanga ni matokeo ya Njaa...kwenye maisha ni vzr kuweka Akiba ya Maneno
 
Aliyezowea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi.
 
Pamoja na yote hayo Ali Choki ni kichwa, ndo maana hata baada ya kuondoka twanga, ile bendi haikuwa kama ilivyokuwa enzi za Ali Choki.

Kama ni kweli ameamua kurudi basi nadhani tutaanza kupata burudani kama zaman kutoka twanga pepeta.
 

Alikuwa anapata ufadhili kutoka kwa mkewe ambae kwa sasa ni marehemu
 
Nimeamini Twanga pepeta ni kisiwa cha burudani

"what goes around, comes round"
 
Hii imefurahisha sana na kuwa funzo kwelikweli kwa kitendo cha mkurugenzi wa extra bongo kurejea ktk band ya Twanga pepeta,ikumbukwe hapo nyuma huyu bwana aliapa hatorejea tena ktk band ile hadi kifa na hata siku akifa mkurugenzi wa Twanga mamaa Asha Baraka asifike katika msiba wake!sasa juzi Choki ametamka mbele ya waandishi wa habari kua yeye Atafia katika band ya Twangapepeta!!kweli tunaishi kwa kujifunza!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…