Ali Choki na Super Nyamwela warudi Twanga Pepeta

HA HA hahaha Choki si ana bendi yake? iweje uhame nyumbani mwako uende kupanga?
Kala matapishi yake ,alipoondoka alimnanga mmiliki wa bendi na bendi yenyewe akajinasibu kuwa hata iweje hawezi rudi Twa,akajisahau kuwa yeye ni mwaajiriwa tu hata hata huko Extra Bongo,kuendesha bendi au kampuni si mchezo jamani,uajiri watu,uwalipe mishahara,NSSF bado TRA wapo nyuma wanakufuata,waswahili husema usitukane mamba ungali hujavuka mto.
 
Njaa ni adui wa kwanza wa mwanadamu
Mkuu njaa inakufanya hata umwamkie shikamoomzee mjukuu wako,lakini pia hili la Choki lafaa liwe fundisho kwa wengine,unapotoka au unaacha kazi sehemu ondoka kwa ustaraabu,usidhani sababu umepata kwingine kuzuri ndio udharau ulikotoka,huyu Choki aliondoka kwa nyodo na kebehi kibao sasa kiko wapi?hii tabia wanazo sana hawa pacha wawili Choki na Muumini sijui sababu wapo pamoja muda mrefu ndio maana tabia zao zinafanana,mara nyingi hupenda kujiapiza hasa wanapogombana au kuondoka kwa Asha Baraka,na nikma vile Asha Baraka anawajua yeye anakaa kimya anajua tu njaa zao zitawarudisha tena Twanga na kweli mara watoke kwa mkwara na baadaye wanarudi wakiwa wamufyata kama mbwa kaona chatu.
 


wengine ni carlo ancellot, roberto mancini , dunga etc, ila in general ulichosema ni kweli
 
😆😆😆😂😂😂😂
 
Choki pamoja na yote bado ni jembe. Sisi tunataka burudani hayo mengine shauri yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…