Lyambalyetu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2021
- 278
- 255
Ali Hapi ambaye anatoka familia ya Mzee Ugula katika kijiji cha Tutu, Kata ya Kiomboi, Wilayani Iramba amekuwa na safari nyingi za kumtembelea bibi yake Mzaa Mama kijijini hapo na safari ya mwisho aliyoifanya na kupiga picha na bibi huyo inasemekana imezalisha jicho la kuonwa na mama na kupewa Nafasi ya Ukatibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi. Hii yote ni kutokana na Ali Hapi kuonwa anawajali sana wazazi na anaweza kuwatumikia vema.
Hata hivyo mtazamo mkubwa uliopo ni Ali Hapi kuanza kutengeneza network hapo kijijini na Kiomboi Mjini ambako ameshapata namba za Viongozi wa CCM katika Kata 7 ambazo anategemea kuanza nazo katika kujitambulisha vizuri akitarajiwa kuleta upinzani mkali dhidi ya Dkt. Mwigulu ndani ya Chama.
Ali Hapi alisikika akitamaka wazi kuwa yeye ni muumini wa vipindi viwili vya ubunge zaidi ya hapo Mbunge huyo anakuwa hana jipya.
Hili linaonekana wazi kuwa lilikuwa ni ndogo dhidi ya Dkt. Mwigulu ambaye ameshatumikia vipindi vitatu katika Jimbo la Iramba.