Uwoga ni dhambi
Member
- Jul 31, 2026
- 18
- 61
Yaani unawaita CHADEMA ni "watukutu wenye pepo mchafu" halafu unataka waitikie wito wa mazungumzo!
Leo Agosti 12, 2026, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa, Ally Hapi, ametoa kauli akiwa Kilosa mkoani Morogoro akiwataka Maaskofu wa TEC kuwaombea viongozi watukutu wa CHADEMA ili "pepo mchafu awatoke" na wakubali wito wa Rais, huku ukiwabeza na kuwaita wana "pepo mchafu" halafu hapo hapo unatarajia wakubali kukaa mezani na kufanya mazungumzo ya maridhiano?!
Nimkumbushe Bwana Hapi kwamba mwezi mei mwaka 2022 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilianza rasmi kushiriki kwa nyakati tofauti katika michakato ya mazungumzo ya maridhiano na serikali ya CCM, Lakini baadae CHADEMA ilibainisha kuwa CCM iliyachinjia baharini mapendekezo yao yote ya kimaandishi yaliyolenga kuleta mabadiliko ya kweli ya kidemokrasia kwa maslahi mapana ya Taifa.
Maswali ya Msingi ni haya.
Mbona kabla ya uchaguzi wa 2025 CCM mlikataa kufanya mazungumzo yoyote na CHADEMA?
Mlisema uchaguzi ulikuwa wa wazi, huru na wa haki. Mkaingia katika uchaguzi na tule tuvyama tule, na baadae mkasema mmeibuka washindi kwa zaidi ya asilimia 97. Kama kweli mlikuwa na uhalali huo mkubwa wa kisiasa, kwa nini leo mnapita nchi nzima kuitajataja CHADEMA na kulialia kuhusu maridhiano?
Kama mliweza kuingia kwenye uchaguzi bila CHADEMA, mkashinda kwa asilimia 97 mliyoitangaza, kwa nini leo msisonge mbele na tule tuvyama twingine pasipo kuihusisha CHADEMA?
Kama CHADEMA haikuwa na umuhimu kabla ya uchaguzi, kwa nini imekuwa muhimu sana baada ya uchaguzi?
Ni kweli, maridhiano ni jambo jema kwa ajili ya kufikia muafaka na kulinda maslahi mapana ya taifa. Hata hivyo, kama CHADEMA inaona wazi kwamba mazingira bado ni yaleyale, na kwamba kutokana na kutokuwepo kwa nia ya kweli hali inayoweza kupelekea maazimio na mapendekezo yake kukataliwa kama ilivyowahi kutokea awali, je, ni lazima chama hicho kuitikia wito na kushiriki katika maridhiano?
Kupitia Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mhe John Heche, chama hicho kimesisitiza kuwa hakitashiriki mazungumzo ya maridhiano bila masharti makuu matatu:
1. Kuachiwa huru kwa Mwenyekiti wao Mhe Tundu Lissu,
2. Kufutwa kwa kesi dhidi ya viongozi na wanachama wa chama hicho.
3. Kuwepo kwa msuluhishi wa kimataifa.
Muda ni hakimu wa mambo yote, Tusisahau kwamba hata juzi ilikuwa mwaka kesho, Tuendelee kunywa Mbege machicha tutayakuta chini. (Imeandikwa na Sir Major wa X)