Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ah yaani wewe unajua leo,jamaa walianza kumgonga muda mrefu sana,aliponzwa na macho matatuHivi alii komwe hapakuliwi kweli yule?
PumbaUSHAURI WA ALLY KAMWE KWA AHMED ALLY.
Shida ni kwamba .. Timu inaposhinda Msemaji unajimilikisha ushindi huo. Unatamba nao na kujipa kila aina ya majina kuonyesha kwamba Wewe ni KILA KITU kwenye Ushindi.
Lakini timu inapopata matokeo mabaya, Unajitenga nayo. Unaanza kutupa lawama hadharani kwa wachezaji kuwa hawana Ubora na Uchu wa kuipa Timu mafanikio.. Huku ni KUKOSA HESHIMA.
Ni Ubinafsi na unaonyesha ni kwa kiasi gani Msemaji upo kwa ajili ya kulijenga jina lako na sio kuijenga Taasisi yako. Na hii ni mbaya pindi Interest binafsi zinapotangulia kuliko Interest za Taasisi.
Jambo moja ambalo inatupasa tuelewe, Nyakati nzuri na mbaya ni kwa ajili ya wote. Hakuna mchezaji anayekwenda uwanjani ili apoteze mchezo.
Kuwazodoa na kuwasema hadharani wachezaji wako ni kutaka kuwachonganisha na mashabiki. Ni ishara pia ya kutoheshimu kazi yao.
Na hata inapobidi, wachezaji wakatakiwa kusemwa, mwenye jukumu hilo ni Mkuu wa Benchi la Ufundi, Sio msemaji wa Timu.
Makocha wamekaa Darasani na wakafundishwa jinsi ya kuishi na kuwaelekeza wachezaji. Tuache wafanye kazi yao.
Kuwa Msemaji haimaanishi Wewe Unajua kila kitu. Haimaanishi una nguvu na uwezo wa kukosoa wapambanaji wako Public. Tujue mipaka yetu.
Kesho na keshokutwa wachezaji wakianza kutukanwa mitandaoni na kupigwa mawe na mashabiki barabarani, Tutaanza kusema kuwa tuna mashabiki wapuuzi.. Kumbe ‘Upuuzi’ tunaujenga kwa vinywa vyetu wenyewe..
Huwezi kuonekana Smart kwa kukosoa na kuwasema wachezaji hadharani .. ili kufurahisha kikundi cha watu wachache..
Hii ni mbaya sana, utamalizana na wachezaji kisha kesho utawakosoa viongozi wenzako na kisha utahamia kwa mashabiki.. Mwisho wake huwa mbaya sana.
Tubadilike .. Kinachotupa Umaarufu na majina makubwa mjini ni TIMU sio Vinywa vyetu .. Tujifunze kuheshimu na kuwalinda wachezaji wetu.
Mwenyekiti wa Wasemaji Hapa ..
Ally Kamwe [emoji1593]
#FutbalPlanetUpdatesView attachment 2851509
Ikiwa kweli au sio kweli nini kitabadilika kwenye maisha yakoHivi alii komwe hapakuliwi kweli yule?
Kupoteza wanachama katika kikundi chetu cha wanaume halisiIkiwa kweli au sio kweli nini kitabadilika kwenye maisha yako
Mimi mwenyewe nashangaa. Watu waliotoka kumsema vibaya Benchikha kwa kuweka mabeki 7 mechi na Wydad ili kulinda ushindi leo wanaishauri Simba.Ukiona Utopolo anatoa ushauri kwa Simba jua hana nia nzuri. Huyo ni Tapeli tu wa kutoa ushauri.
Hata tabia zake ana uprofessional nazo?By professional..Ali kamwe ni mchambuzi so anauelewa na Hilo suala
Mwanaume hua hafatilii mambo ya wengine na wewe unaenda huko hukoKupoteza wanachama katika kikundi chetu cha wanaume halisi
Unapo anzishaga threads za kuishauri kwa Yanga hua una maana gani? au ndio nyani haoni dude lakeMimi mwenyewe nashangaa. Watu waliotoka kumsema vibaya Benchikha kwa kuweka mabeki 7 mechi na Wydad ili kulinda ushindi leo wanaishauri Simba.
Yaani wasivyoitakia mema Simba wanapata wapi busara za kumshauri Ahmed Ally na kuwaonea huruma wachezaji wa Simba. Au labda mimi ndiyo sielewi.
Vijana acheni kudharirisha wenzenu kwa huu ujinga.Ah yaani wewe unajua leo,jamaa walianza kumgonga muda mrefu sana,aliponzwa na macho matatu