Ali kamwe alivyowaamsha wachambuzi wa soka walio lala fofofo

Ali kamwe alivyowaamsha wachambuzi wa soka walio lala fofofo

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
Habari za weekend wakuu

Baada ya jana kusambaa video ikimuonyesha waziri mkuu akimsifia ALI KAMWE kwa tathmini yake aliyoifanya juu ya simba kuvaa jezi ikiwa na neno linalosomeka 'VISIT TANZANIA' na namna kama nchi na sekta ya utalii itakavyonufaika na tangazo lile.

Baada ya simba na serikali kuingia makubaliano ya kuvaa VISIT TANZANIA katika jezi wanazotumia katika mashindano ya CAF baadhi ya wachambuzi na wadau mbali mbali wa michezo waliponda na kusema haina tija kwa taifa, kuwaambia wa AFRICA waitembelee Tanzania ila hiyo yote ni kutokana na utani wa jadi wa simba na yanga kila mtu alikuwa anajaribu kuelezea kwa upande.

Ila baada ya Waziri Mkuu kumpongeza ALI KAMWE nadhani wachambuzi na wadau wa soka watajifunza kutoka kwake jinsi ya kuangalia kwa manufaa ya taifa kuliko kiushabiki kama wanavyo fanya kina maulidi kitenge, oscar oscar, na kina gift macha ambao mda wote wanatafuta makosa kuliko uhalisia.
 
unawambia mwafrika mwenye kipato cha kula mlo mmoja visit Tanzania
 
Kwani michuano inatazamwa na waafrika pekee?
99% ni waafrika tena wapenda mpira na hela hawana wanatizama kwenye mabanda umiza tena mechi zinazo wahusu (nchi zao) waliobaki ni wasaka vipaji ambao hawana mda wa kumtizama tshabalala wala morisson wao wanahangaika na timu za afrika magharibi.
 
99% ni waafrika tena wapenda mpira na hela hawana wanatizama kwenye mabanda umiza tena mechi zinazo wahusu (nchi zao) waliobaki ni wasaka vipaji ambao hawana mda wa kumtizama tshabalala wala morisson wao wanahangaika na timu za afrika magharibi.
Uto katika Ubora wenu
 
Nikadhani unaainisha faida zilizotokana na hayo maneno kumbe hoja ni kusifiwa na Majaliwa ambaye naye ni Simba damu. Kauli ya Waziri Mkuu haijibu hoja zilizoibuliwa ila kwa nafasi kaongelea katika muktadha wa uzalendo.
 
Kwamba amemvua Nguo Hadi wazir wa maliasili na utalii 😀
 
Back
Top Bottom