Wadau je ni kweli Ali Kamwe alizuiwa kuingia uwanjani siku ya wiki ya Mwananchi kwa shinikizo la watu kadhaa ndani ya Yanga?
Maana ishu hii imekuwa kubwa sana ikizungumzwa naomba tuizungumze pamoja kumuhusu huyu Meneja wa Habari na Mawasiliano Yanga SC Klabu kubwa Afrika kwa sasa.
Maana ishu hii imekuwa kubwa sana ikizungumzwa naomba tuizungumze pamoja kumuhusu huyu Meneja wa Habari na Mawasiliano Yanga SC Klabu kubwa Afrika kwa sasa.
- Tunachokijua
- Tangu kurejea kwa Haji Manara Yanga kumekuwa na hoja zikidai hakuna maelewano kati yake na aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Habari wa Yanga Ali Kamwe.
Baada ya Tamasha la siku ya Mwananchi kufanyika Agosti 4, 2024 kumekuwa na maswali mengi kutokea kwa Wadau wakidai Ali Kamwe alitengwa na kuzuiliwa kuingia uwanjani siku ya Tamasha hilo.
Kuna ukweli wa Hoja hii?
JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo kwa kuwasiliana na Kamwe mwenyewe ambaye amekanusha uvumi wa yeye kutengwa kushiriki katika tamasha hilo.
Kamwe anasema "Mimi nilikuwepo na nilishiriki kwenye shughuli zote za Klabu. Namshukuru Mwenyezi Mungu Ushiriki wangu na wenzangu umefanikisha Tamasha lililokuwa bora na la kihistoria
Naye, Msemaji wa Klabu Haji Manara amefafanua kuwa Kamwe alitoa mchango mkubwa kuanzia maandalizi mpaka kufanikisha tamasha hilo huku akisema maneno yanayoendelea yanalenga kuwagombanisha.