Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Mpaka SASA Kamwe anadiwa bilioni kumi na nne; Huyu jamaa ataweza kweli kushindana na Sandaland na Azam mahakamani?
Azam FC imempatia taarifa rasmi Afisa Habari wa Yanga SC, Haji Ally Kamwe, kudai fidia ya TZS 10,000,000,000 kwa tuhuma za kuichafua klabu hiyo kwa madai ya kuzima taa uwanjani ili kumzuia Prince Dube kufunga magoli.
Azam FC inadai kuwa kauli hiyo ilitolewa hadharani na Kamwe kupitia vyombo vya habari, na imesababisha madhara makubwa, ikiwemo kupoteza mahusiano ya kibiashara na wadau wake.
Klabu hiyo imetoa muda wa siku 14 kwa Kamwe kutengua kauli zake hadharani, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Azam FC imeeleza kwamba itaendelea kulinda brand yake dhidi ya mtu yeyote au taasisi itakayojaribu kuichafua kwa njia yoyote ile.
Kamwe amekuwa akijulikana kwa kauli zake za moto, lakini suala hili linaweza kuwa hatua mpya kwa migogoro na vilabu vikubwa nchini.