Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 144
BALOZI wa Tanzania nchini Italia ambaye pia ni mtoto wa rais wa kwanza wa Zanzibar, Ali Abeid Karume ameanza kampeni za kuwania kiti cha urais wa Zanzibar kumrithi kaka yake Rais wa sasa wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Amani Abeid Karume.
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili umebaini kuwa Balozi huyo, ambaye kwa sasa yupo hapa nchini, ameanza kampeni za kusaka kuungwa mkono na baadhi ya watu muhimu ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hata hivyo, katika mahojiano na Mwananchi Jumapili, alisema hakuenda Dodoma kwa ajili ya kujifanyia kampeni bali yeye kama Mkuu wa Mabalozi wa Tanzania Nchi za Nje, alienda kama mtaalamu ambaye angeweza kuhitajika wakati wowote kusaidia kutoa ufafanuzi wakati bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ikijadiliwa.
Mwaka 2005 Balozi Ali Karume alikuwa miongoni mwa wanachama wa CCM ambao walikuwa wakiwania kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano ambapo Rais Jakaya Kikwete alishinda nafasi hiyo.
Katika kampeni zake Karume amekuwa akitamka bayana kuwa atajitokeza kuwania kuteuliwa na CCM kugombea Urais visiwani humo kuchukua nafasi ya kaka yake Amani Karume ambaye anamaliza muda wake wa urais Novemba 2010, baada ya kuongoza kwa miaka 10.
Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar, mtu yeyote akichaguliwa nafasi ya rais, haruhusiwi kuongoza kwa zaidi ya miaka 10.
Akiwa mjini Dodoma, Balozi Karume alikutana na wabunge mbalimbali wa CCM, miongoni wakiwamo wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) pamoja na Kamati Kuu ya chama hicho (CC).
Mwananchi lilimshuhudia akifanya mazungumzo na viongozi mbalibali wenye ushawishi ndani ya chama katika viwanja vya bunge.
Ni kweli amekutana nami, lakini mambo haya yalikuwa mazungumzo baina yangu naye na ameniomba nimuunge mkono kwa vile atagombea Urais wa Zanzibar. Nilimsikiliza sasa kama nitamuunga mkono ama laa hiyo ni juu yangu alieleza mmoja wa viongozi ambaye alikutana na Karume na kuombwa kumuunga mkono kwa sharti la kutotajwa jina.
Mwananchi Jumapili lilipowasiliana kwa njia ya simu na Karume, alisisitiza ukweli wa nia hiyo ya kuwa rais wa Zanzibar kipindi kijacho, lakini akakanusha kuwa alienda Dodoma kufanya kampeni.
"Hiyo siyo kweli kabisa. Napenda kwanza ufahamu kuwa mimi ni Mkuu wa Mabalozi wote wa nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," alisema Karume akifafanua:
"Mimi nilienda kule kuona jinsi mijadala ilivyokuwa inaendeshwa na pili nilikuwa kama mshauri iwapo lingejitokeza suala linalohusu mambo ya kibalozi wakati inajadiliwa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa."
Alibainisha kuwa kama ni suala la kampeni basi angelifanya wakati ambapo mkutano wa NEC au CC unakaribia.
Alipotakiwa kueleza kama haoni kama akichaguliwa Itaonekana uongozi wa Zanzibar ni wa kupokezana kama ule wa Kisultani, alipinga akisema utawala wa namna hiyo kwa kawaida baba humrithisha mwanaye na siyo ndugu.
"Nalizungumzia hili kwa sababu wengi wamekuwa wakilihoji. Kama ungekuwa ni utawala wa namna hiyo basi Rais Amani angemrithisha mwanaye. Tena anao wakubwa na wenye uwezo wa kupewa nafasi iwapo utawala ni wa namna hiyo."
Anasema utawala wa kurithi ni ule wa baba kumuachia mtoto uongozi na kueleza kuwa hakuna urithi wa utawala kutoka kwa kaka kwenda kwa mdogo mtu, hivyo uamuzi wake wa kugombea usitafsiriwe katika maana hiyo, alieleza Mbunge mmoja huku akimnukuu Balozi Karume maelezo yake.
Amekuwa akieleza kuwa kugombea ni haki alisema kuwa yeye anagombea kwa sababu anajua anao uwezo hasa ikizingatia kuwa, ana elimu ya kutosha pamoja na uzoefu mkubwa wa kimataifa.
"Mimi ni Mzanzibari mwenye uzoefu wa muda mrefu wa uongozi ndani na nje ya nchi. Nimekuwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda kwa miaka sita. Nina elimu ya kutosha, nimesoma Marekani taaluma ya siasa na uchumi. Ninayo shahada ya uzamili.
"Nimekuwa na uzoefu wa uongozi kimataifa kwa kuwa balozi wa Tanzania nchi mbalimbali na sasa mimi ni Mkuu wa Mabolozi wa Tanzania nchi za nje."
Kutokana na hali hiyo alisema amejiona ana sifa zote za kuwaongoza Wazanzibar na amekusudia mambo mengi yenye manufaa kwao.
Uchunguzi unaonyesha kuwa hata baadhi ya wabunge wanamuunga mkono kwa kile wanachoeleza kuwa katiba ya nchi inampa haki ya kuchaguliwa kiongozi mtu yeyote bila kubagua kuwa ni mtoto au ndugu wa kiongozi aliyewahi kushika wadhifa huo.
Cha msingi, baadhi ya wabunge hao ambao hawakupenda majina yao yatajwe, walisema kuwa jambo la muhimu ni kama katiba inamkubali na pili ni sifa zake za uongozi.
Karume alipoulizwa juu ya vuguvugu la kero za muungano ambalo linaashiria kuuvunja, alisema anaheshimu sana mambo yote yaliyoasisiwa na baba yake, Abeid Karume.
Hivyo, akasema akiwa rais moja ya mambo ambayo atayalinda kwa nguvu zote, la kwanza ni kutetea mapinduzi hadi dakika ya mwisho na pili ni kulinda muungano.
Alisema chokochoko za muungano ni za kawaida kwa sababu popote duniani ambako kuna muungano wa nchi na hata majimbo, malalamiko ya hapa na pale hayakosekani.
"Hata Tanganyika ilipopata uhuru, baadhi ya mikoa kama vile kule Rukwa, walilalamika kuwa hawapati haki Hata kule Marekani ambako kuna muungano ambao unaonekana kuwa imara, yapo majimbo ambayo yanalalamikia muungano," alibainisha Karume.
Kwa sababu hiyo alisema dawa si kuvunja muungano bali ni kutatua kero zinazojitokeza.
Alipoulizwa kama tatizo ni muundo wa muungano ambao umezaa serikali mbili, alionya kuwa zikiundwa serikali tatu, mvutano unaweza kuwa mkubwa zaidi na kulisambaratisha taifa.
Alisema kuwa muundo wa serikali mbili au moja, ndio unaoweza kuwa imara na wenye manufaa.
Alisema kuwa Wazanzibar wengi wanaunga mkono muungano kwa sababu una manufaa mengi kwao.
SOURCE: MWANANCHI