Ali Karume Aanza Kampeni za Urais Zanzibar

URAIS WA ZANZIBAR A.K.A VIBARAKA WA KULINDA MAUWAJI YANAYOITWA MAPINDUZI 1964 NA UNYONYAJI,UKUPE,UKOLONI NA WIZI UNAOITWA MUUNGANO.
1. Amani A. Karume 2000-2010
2. Ali A.Karume 2010-2020
3. Ahmed A.A. Karume 2020-2030
4. Fatma A.A Karume 2030-2040(siku hizo watasema zamu ya mw'mke)
5. Mansour Yussuf Himid 2040-2050
6. Hussein Ali Hassan Mwinyi 2050-2060
7. M. H. Nassor Moyo 2060-2070
8. Amin Salmin Amour 2070-2080(huyu anaweza akabadilisha katiba aongeze muda)
9. Mustapha Aboud Jumbe 2080-..........
0..............................

.......................................
....................................
...................................
n.k kama watakuwa na watoto wao na wao watawarithisha.

This is so called Neo - sultanism
 
Hiki ni kipindi cha watu wa mujini, mambo ya Kaskazini, Kusini ama Kisiwa cha pili waendelee kusubiri tu...


Rais karume na timu yake wanamjuwa nani wanamtaka awe rais na sio vyenginevyo wabunge waliupata ujumbe wa SMZ wakati ule wa mapatanisho na kusalenda, timu ile kwa mara nyingine tena itatumia zana nzito safari hii la sihivyo wanarudi nyumbani na kitu kinachoitwa kisiwanduwi (ASP)kazi kwenu .
 


Duh, Ungetuletea huo ushahidi ungetusaidia kweli!!!!
 
Yap wakati wa mjini ila sio baghani au shangani mjini n'gambo au sio kaka yangu kibunango
 
Ni haki ya kila mzanzibari mwenye sifa kugombea kwa hio mie naona hakuna tatizo juu ya hilo wanaopinga wana yao mengine

waamuzi ni wanachama kwa ngazi ya chama na wananchi kwa ngazi ya nchi
 
😀 😀
Haya!
 
Kwani Bi.Mkubwa keshatowa tamko, maana alilia siku ile kwa Mkapa mwanawe apewe kipindi kingine, sasa zamu ya Ali, je Bimkubwa atakwenda Bumbwini kwa wataalamu wake kuweka mambo sawa.
 
Huyu nitamfagilia kwa sababu mbili. Kwanza ni rafiki yangu na pili anataka kudumisha mwungano.
Kaka kweli demokrasia ipo mwache agombee, maana majority ndio watakaochangue.
Kibaya kama fedha ipo basi Dodoma wale wazee watagombea hayo mafungu na kumpitisha.
K. Gwamaka
 

Mkuu Junius,
Mimi naona huyu ndie anaefaa kwa miaka kumi ijayo. Duru la kwanza limekwisha tumeshaanza na watoto na kwa sabau RAHISI wa pili alikuwa Jumbe yafaa mtoto wake achukue nji. Kisha mtoto wa mwinyi, halafu Idrisa na Kisha Salmin. Baada ya hao wanafuata watoto wa Aman, Mustapha and the list goes on mpaka kiama.
 
Jumbe? Kule Shakani, Buju na kona zote za tende lazima wataamdamana kupinga uteuzi wake.
 
Jumbe? Kule Shakani, Buju na kona zote za tende lazima wataamdamana kupinga uteuzi wake.

Katika desperation waliyonayo wanzibara kuhusu Muungano wako tayari kumchagua mtu yeyeyote atakayewaahidi kuwatoa katika "himaya ya mkoloni Tanganyika." Si ni Jumbe Senior aliyetaka kuhitimisha Muungamo?
 
Katika desperation waliyonayo wanzibara kuhusu Muungano wako tayari kumchagua mtu yeyeyote atakayewaahidi kuwatoa katika "himaya ya mkoloni Tanganyika." Si ni Jumbe Senior aliyetaka kuhitimisha Muungamo?
Tatizo si muungano kwa Jumbe, bali ni msimamo wake katika social life ya Zenj!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…